Pichani ni Ndugu Absalom Kibanda akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha matibabu,hospitali ya Taifa Muhimbili.Get Well soon Absalom Kibanda.Picha kwa hisani ya Mtandao wa Mabadiliko.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri,na Mhariri Mkuu wa Mtendaji wa New Habari Coperations Ltd, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa usiku  wa kuamikia leo akiwa anashuka nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wasiofahamika na kumpiga kichwani. Amepata majeraha Makubwa kichwani na hasa jichoni,aidha taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo Kibanda alikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu.

Wadau hii ni taarifa ya kushtua sana,lakini tutazidi kutaarifiana kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana,kikubwa tumwombee Mungu amponye haraka mpiganaji mwenzetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. BUNGE NI LAZIMA LIONYESHWE MOJA KWA MOJA KTK RUNINGA!

    Ili tuendelee ni lazima tukubali kukosoana na kuwajibishana, ni kama alivyotoa Mhe.James Mbatia kuhusu Mitaala mibovu ya Elimu, akapingwa na majibu ya ubishi huo ni Matokeo mabovu Mitihani ya Kidato cha nne.

    Hata kama Mhariri Absalom Kibanda amejeruhiwa hilo sio suluhisho tunajua ni kwa msimamo wa Bunge kuonyeshwa live kwenye Runinga!

    ReplyDelete
  2. Bongo imeoza, huyu naye amemkosea nani. What is the actual problem in bongo kuuana na kupigana kiasi hicho. Pole sana and I hope you will et through this.

    ReplyDelete
  3. Rwanda ya zamani yatua Bongo?

    ReplyDelete
  4. get well soon

    ReplyDelete
  5. Kweli mpaka sasa hakuna maoni yeyote ina maana hamna aliyeshtuka na hii maneno.Au hatupendani jameni hasa nyie waandishi wa habari.Haiwezekani hatulaani hii matendo ya kinyama sasa vipi kakosa huyu mpaka apigwe na kujeruhiwa hivyo.sheria ichukue mkondo na hao waharifu watafutwe upesi.

    ReplyDelete
  6. Prof. Lyamba lya MfipaMarch 06, 2013

    'rada' yangu inasema kuna 'mkono wa mtu' Pole sana Kibanda.

    ReplyDelete
  7. Nani kafanya unyama huu? hapa ndipo ninapomkumbuka kamanda ras makunja na vichaa ngoma africa ule wimbo wao
    !Uhuru wa habari, machizi darubini yao iliona mbali

    ReplyDelete
  8. Get well soon..... Pole kwako familia na wanahabari wote. Mwenyezi MUNGU akupe akuponye na kukupa uzima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...