Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti Muzdalifa,Sheikh Abdalla Hadhal,alipoangalia maonesho ya picha mbali mbali wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Yatima katika Ukumbi wa Salama Bwawani leo, maadhimisho hayo yamefanywa na Shirika la I.H.H la nchini Uturuki kwa ushirikiano na Jumuiya ya Muzidalifa ya hapa Zanzibar inayoshuhulika kna Mayatima.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa Mtoto Hinaina Said Khalfan,wakati wa sherehe za siku ya Mtoto yatima zilizofanyika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel leo Mjini Zanzibar,shirika la misaada la I.H.H la Uturuki,kwa Ushirikiano na jumuiya ya Muzdalifa ya hapa Zanzibar kwa pamoja wamefanikisha kufanyika kwa sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa Sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto Yatima katika ukumbi wa Salama bwawani Mjini Zanzibar leo,maadhimisho hayo yamesimamiwa na jumuiya ya Muzidalifa na Shikika la misaada la I.H.H la Nchini Uturuki,(kushoto) makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Balozi wa Uturuki Nchini Ali Daudi Gul,na Waziri wa Katiba na Sheria,Abubakar Khamis Bakary,(kulia).
Watoto Yatima waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Mtoto Yatima,wakiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar,zilipofanyika sherehe hizo,kwa ushirikiano wa jumuiya ya Muzdalifa na shirika la misaada la I.H.H la Nchini Uturuki leo na kuhudhuriwa na wananchi na Viongozi mbalimbali.

BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...