Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kimeanzisha program mpya ya Diploma ya Juu ya Elimu iliyoanza chuoni hapo hivi karibuni. Programu hiyo inatolewa massa ya jioni na ina lenga kuwapa fursa watu ambao wangependa kujiendeleza katika taaluma ya ualimu lakini hawana muda wa kujiunga na masomo katika muda wa kawaida. 

Programu hii inatolewa kwa watu ambao wana shahada au stashahada katika fani nyingine nje ya ualimu lakini wangependa kujiunga na taaluma ya ualimu au tayari wanafundisha lakini hawakusomea ualimu. Progranu hii pia inawafaa watu wanaoendesha shule kama wamiliki au viongozi wa shule.
Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Dkt Kitila Mkumbo akitoa maelezo yanayohusiana na program mpya ya Diploma ya Juu ya Elimu inayosimamiwa na kitivo cha Elimu, kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Profesa Godliving Mtui.
Naibu Mkuu wa chuo (Taaluma), Profesa Godliving Mtui akikabidhi makabrasha mbalimbali kwa wanafunzi wapya wa Diploma ya Juu ya Elimu ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa program hiyo.
Wanafunzi wapya wa Diploma ya Juu ya Elimu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa program hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Bravo,bravo,bravoooo,nikama vile mlichelewa kuianzisha,tupeni maelekezo ya kujiunga.

    ReplyDelete
  2. its a good move in the right direction!nafikiri hata sekta nyingine hapa nchini zenye critical shortage ya staff wangeiga mfano huu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...