Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo yaliyofanyika kwa wiki tatu.
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani leo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi kutoka kwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. 
Zote za Tanga na Hussein Semdoe.
wakwanza katika mstari wa kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefuata ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, wakiwa kwenye Paredi ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kikosi cha 835 Mgambo JKT kambi iliyopo katika Kata ya Mgambo ilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
wakwanza kushoto ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ZItto Kabwe, wakihitimu mafunzo ya JKT katika kambi ya 835 Mgambo JKT iliyopo Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Biharamulo, Dk Athanas Mbassa, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. 
Mbunge wa Kiwani Pemba, Abdallah Haji Ali, , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akiapa mbele ya kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu, hayupo pichani, wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge Viti maalum Raya Khamis , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni.
Baadhi ya Wabunge walikuwa wakichukua mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa wabunge waliohitimu mafunzo maalumu ya JKT leo

Mbunge wa Mtera Mh. Livingstone Lusinde 
"Kibajaji"  (wa tatu toka kulia) akipiga kwata leo huko Ruvu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. huu ni utani eti mafunzo ya siku tatu jkt wakati sisi ilikuwa mwaka mmoja!!

    ReplyDelete
  2. Saafiiiiiiii saaaaanaaaa!

    Duhhh Serikali kweli baba!

    Ni uamuzi wa Busara sana kuyarudisha mafunzo ya JKT nchini!

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza Mafunzo wamepewa ya wiki tatu (3 weeks) hiyo kulingana na Majukumu yao inatosha kabisa!

    Lakini si haba inatosha sio sawa na kutokwenda mafunzoni kabisa, nadhani wamepewa mambo muhimu kwa ufupi.

    Nakumbuka zamani sana ilikuwa mwaka mmoja lakini mwishoni miaka ya karibia kufungwa mwaka 1994 ikawa ni miezi 6 tu.

    JKT mchezo?

    ReplyDelete
  4. Hii ni nzuri mfano mzuri wauzalendo wabunge wetu wameonyesha. Inabidi uendelele mpaka kuweka interest za utaifa mbele.

    ReplyDelete
  5. Wiki 3? Mie niliepiga mwaka mzima? Miezi sita kuruta na 6 service man. Havilingani. Sembe mwaka mzima.

    ReplyDelete
  6. Hongereni viongozi wetu kwa kuhitimu! Vyovyote iwavyo, na waseme utani, wasiojali majukumu yenu n.k. mmeonyesha mfano. Kwa serikali: Tupo watu tuliokuwa tayari kwenda JKT na bahati mbaya mpango huo ukasimamishwa wakati wengine tukijiandaa kwenda 1994, je serikali inampango wowote wa kutufikirai watu tunaoona umuhimu wa kwenda kwa hiyari kupata nafasi hiyo?


    sesophy

    ReplyDelete
  7. raha zaidi ni pale wameweza kupata opportunity ya kufanya mazoezi. Natumaini walipewa pia mafunzo ya afya ya kuzuia magonjwa sugu ya moyo, kisukari, n.k kwani watanzania bado tunafikiri kuwa navitambi ni afya

    ReplyDelete
  8. Mgambo....835KJ, mwaka mmoja..DIET MACHUNGWA...starehe KABUKU NJE...oops miongo michache iliyopita

    ReplyDelete
  9. Naona waheshimiwa Wabunge wametofautishwa kwa magwanda meaning walikuwa treated tofauti na wengine, hio haikukaa vizuri.

    ReplyDelete
  10. Ohhh Serikali funiko!

    Yaani na ubishi wao imebidi wenyewe waripoti Kambini?

    1.Je, simu zao walikwenda nazo ama walipowasili Kambini waliamriwa kuzizima na kuzikabidhi kwa Maafande?

    2.Je, magari walipaki wapi au walikwenda kuripoti kwa usafiri wa mabasi?

    3.Kila kitu kinawezekana, hamkumbuki Mjomba Michuzi aliturushia picha ya mwaka 1984 Wabunge wanasafiri kwenda Dodoma Bungeni kwa Bus la Leyland CD?, TENA LENYE VITI VYA KATA SHINGO?

    ReplyDelete
  11. Sawa sawa!,

    Nadhani hili zoezi la Waheshimiwa Makambini liwe ni la kudumu, iwe ni kama sehemu ya Uongozi kwenda Kambini mara angalau moja baada ya miaka 2 au 3 hivi.

    Itafaa pia Spika anapowawajibisha Wabunge wakorofi sio kuwafungia kuhsiriki Bunge kwa kipindi fulani pekee bali adhabu ingine wakatumikie muda wa Kambini Jeshini.

    Ndio tutawajenga ili watuhudumie kama Viongozi wazalendo na waliokomaa na sio kuwa na vitambi vya manyama choma ya Mnadani Dodoma!

    ReplyDelete
  12. Nimefurahi kuona mzee Kikwete kaenda na mama Salma Ruvu mama salma atakua anakumbuka enzi zetu Ruvu naona imemkumbusha mbali sana namsifu ni mpiganaji huyo wasimuone hivyo alipiga mwaka Ruvu
    Mheshimiwa zito na wenzako hongera sana mmeonyesha ujasiri, ukakamavu na uwezo mkubwa kwa wasiojua huko mahala sio masihara siku moja kama mwaka

    ReplyDelete
  13. Siku tatu sasa haya ni mafunzo gani!! Hata raha ya Jeshi hawajaiona hawa; Siku ya kwanza Orientation, siku ya pili kuchukua uniforms na siku ya tatu kuonana au kutambulishwa kwa CO!! Hawajakata kuni; hawaja "jongo" hakuna minazi!!! hata allowance ya 1000Tsh. hawaja qualify kupata; hawalinda guard!! Hivi hata kwenye kuni wameenda kweli hawa? Hawaja enda kwenye mabanda ya kuku kufagia na kulisha kuku; Kweli wamemiss sana!! Afande hebu wape AJUAHH warudie tena...

    ReplyDelete
  14. Afande Ajuah!! Hawasimamisha minazi hao....

    ReplyDelete
  15. Nimecheka sana. Wanaikua mestini? Unanywea uji unapigia pasi nguo,unatumia kama mto, unaogea? Je bukta wamevaa? Au wsmeanzia uservice man. Wameimba disco?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...