Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo yaliyofanyika kwa wiki tatu.
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani leo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi kutoka kwa kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo
ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa
Tanga.
Zote za Tanga na Hussein Semdoe.
Zote za Tanga na Hussein Semdoe.
wakwanza katika mstari wa kushoto ni Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe anayefuata ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, wakiwa
kwenye Paredi ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kikosi cha
835 Mgambo JKT kambi iliyopo katika Kata ya Mgambo ilayani Handeni Mkoa wa
Tanga.
wakwanza kushoto ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani pamoja na Mbunge
wa Kigoma Kaskazini, ZItto Kabwe, wakihitimu mafunzo ya JKT katika kambi ya
835 Mgambo JKT iliyopo Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya
JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu
wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Biharamulo, Dk Athanas Mbassa, akiapa wakati wa kumaliza
mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya
Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kiwani Pemba, Abdallah Haji Ali, , akiapa wakati wa
kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika
Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akiapa mbele ya kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu, hayupo pichani, wakati wakimaliza mafunzo
ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa
Tanga.
Mbunge Viti maalum Raya Khamis , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya
JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu
wilayani Handeni.
Baadhi ya Wabunge walikuwa wakichukua mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. |
huu ni utani eti mafunzo ya siku tatu jkt wakati sisi ilikuwa mwaka mmoja!!
ReplyDeleteSaafiiiiiiii saaaaanaaaa!
ReplyDeleteDuhhh Serikali kweli baba!
Ni uamuzi wa Busara sana kuyarudisha mafunzo ya JKT nchini!
Mdau wa kwanza Mafunzo wamepewa ya wiki tatu (3 weeks) hiyo kulingana na Majukumu yao inatosha kabisa!
ReplyDeleteLakini si haba inatosha sio sawa na kutokwenda mafunzoni kabisa, nadhani wamepewa mambo muhimu kwa ufupi.
Nakumbuka zamani sana ilikuwa mwaka mmoja lakini mwishoni miaka ya karibia kufungwa mwaka 1994 ikawa ni miezi 6 tu.
JKT mchezo?
Hii ni nzuri mfano mzuri wauzalendo wabunge wetu wameonyesha. Inabidi uendelele mpaka kuweka interest za utaifa mbele.
ReplyDeleteWiki 3? Mie niliepiga mwaka mzima? Miezi sita kuruta na 6 service man. Havilingani. Sembe mwaka mzima.
ReplyDeleteHongereni viongozi wetu kwa kuhitimu! Vyovyote iwavyo, na waseme utani, wasiojali majukumu yenu n.k. mmeonyesha mfano. Kwa serikali: Tupo watu tuliokuwa tayari kwenda JKT na bahati mbaya mpango huo ukasimamishwa wakati wengine tukijiandaa kwenda 1994, je serikali inampango wowote wa kutufikirai watu tunaoona umuhimu wa kwenda kwa hiyari kupata nafasi hiyo?
ReplyDeletesesophy
raha zaidi ni pale wameweza kupata opportunity ya kufanya mazoezi. Natumaini walipewa pia mafunzo ya afya ya kuzuia magonjwa sugu ya moyo, kisukari, n.k kwani watanzania bado tunafikiri kuwa navitambi ni afya
ReplyDeleteMgambo....835KJ, mwaka mmoja..DIET MACHUNGWA...starehe KABUKU NJE...oops miongo michache iliyopita
ReplyDeleteNaona waheshimiwa Wabunge wametofautishwa kwa magwanda meaning walikuwa treated tofauti na wengine, hio haikukaa vizuri.
ReplyDeleteOhhh Serikali funiko!
ReplyDeleteYaani na ubishi wao imebidi wenyewe waripoti Kambini?
1.Je, simu zao walikwenda nazo ama walipowasili Kambini waliamriwa kuzizima na kuzikabidhi kwa Maafande?
2.Je, magari walipaki wapi au walikwenda kuripoti kwa usafiri wa mabasi?
3.Kila kitu kinawezekana, hamkumbuki Mjomba Michuzi aliturushia picha ya mwaka 1984 Wabunge wanasafiri kwenda Dodoma Bungeni kwa Bus la Leyland CD?, TENA LENYE VITI VYA KATA SHINGO?
Sawa sawa!,
ReplyDeleteNadhani hili zoezi la Waheshimiwa Makambini liwe ni la kudumu, iwe ni kama sehemu ya Uongozi kwenda Kambini mara angalau moja baada ya miaka 2 au 3 hivi.
Itafaa pia Spika anapowawajibisha Wabunge wakorofi sio kuwafungia kuhsiriki Bunge kwa kipindi fulani pekee bali adhabu ingine wakatumikie muda wa Kambini Jeshini.
Ndio tutawajenga ili watuhudumie kama Viongozi wazalendo na waliokomaa na sio kuwa na vitambi vya manyama choma ya Mnadani Dodoma!
Nimefurahi kuona mzee Kikwete kaenda na mama Salma Ruvu mama salma atakua anakumbuka enzi zetu Ruvu naona imemkumbusha mbali sana namsifu ni mpiganaji huyo wasimuone hivyo alipiga mwaka Ruvu
ReplyDeleteMheshimiwa zito na wenzako hongera sana mmeonyesha ujasiri, ukakamavu na uwezo mkubwa kwa wasiojua huko mahala sio masihara siku moja kama mwaka
Siku tatu sasa haya ni mafunzo gani!! Hata raha ya Jeshi hawajaiona hawa; Siku ya kwanza Orientation, siku ya pili kuchukua uniforms na siku ya tatu kuonana au kutambulishwa kwa CO!! Hawajakata kuni; hawaja "jongo" hakuna minazi!!! hata allowance ya 1000Tsh. hawaja qualify kupata; hawalinda guard!! Hivi hata kwenye kuni wameenda kweli hawa? Hawaja enda kwenye mabanda ya kuku kufagia na kulisha kuku; Kweli wamemiss sana!! Afande hebu wape AJUAHH warudie tena...
ReplyDeleteAfande Ajuah!! Hawasimamisha minazi hao....
ReplyDeleteNimecheka sana. Wanaikua mestini? Unanywea uji unapigia pasi nguo,unatumia kama mto, unaogea? Je bukta wamevaa? Au wsmeanzia uservice man. Wameimba disco?
ReplyDelete