Mshauri Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,James Rugemarila (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya uhalali wa usambazaji wa Bia za Windhoek zinazotengenezwa na Kampuni ya Namibia Breweries,leo kwenye Ukumbi wa Elkad 24,Mikocheni jijini Dar.Hali hii imekuja kutokana na kujitokeza kwa wafanyabiashara wanaoingiza baadhi ya bidhaa kwa njia za magendo, hali inayoikosesha serikali mapato kwa kiasi kikubwa. Wafanyabiashara hao wasiowaaminifu wamekuwa wakiingiza bia hiyo ya aina ya Windhoek kwa njia za magendo ili kukwepa kulipa ushuru halali wa serikali na kuikosesha mapato ambayo yangetumika katika miradi mingi ya maendeleo.Wengine pichani ni toka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,Benedictor Rugemarila,Meneja Mkuu wa Mabibo,Neil Stainton pamoja na Mshauri wa Mambo ya Usalama na Sheria wa Mabibo,Kamala Stephen.
Meneja Mkuu wa Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,Neil Stainton akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wakitoa taarifa ya uhalali wa usambazaji wa Bia za Windhoek zinazotengenezwa na Kampuni ya Namibia Breweries,leo kwenye Ukumbi wa Elkad 24,Mikocheni jijini Dar.Kulia ni Mshauri Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,James Rugemarila.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,Benedictor Rugemarila akionyesha namba maalum (inayosomeka MB 66) iliopo kwenye chupa ya Bia ya Windhoek inayoitambulisha Kampuni yake kuwa ndio yenye uhalali wa kusambaza vinywaji hivyo hapa nchini.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hii ni biashara huria banaa..kwa nn wao wawe wasambazaji pekee???biashara hizo zilikua enzi hizo sio sasa...ushindani muhimu kukidhi haja ya mnywaji...wasihodhi usambazaji..hii ni karne ya 22 atii..
    Mdau wa London

    ReplyDelete
  2. Mzee mzima vipi ina maana yule bwana mdogo wa Kibosho "kakuvurumisha" hadi umekimbia bia ya Heineken?

    Hebu tupashe Mulangira kama ni kweli umesalimu amri kwa bwana mdogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...