Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa ameongoza maelfu ya Wakazi wa mji wa Arusha na mikoa ya jirani katika mazishi ya mfanyabiashara na Kada maarufu wa CCM Mkoani Arusha,Marehemu Henry Nyiti,nyumbani kwake Tengeru Arusha .

Nyiti alifariki ghafla wiki iliyopita akiwa katika mgodi wake wa madini,Mahenge Mkoani Morogoro.

Wengine walioudhuria katika mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu,Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dr. Reginald Mengi,Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo,Mwenyekiti wa Chadema,Mh. Freeman Mbowe na Ridhiwani Kikwete.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongoza viongozi wenzake kwenda kwenda kuweka udongo kaburini.nyuma yake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.

Mwenyekiti wa makampuni ya IPP,Dr. Reginald Mengi naye akiweka udongo kaburini.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka shada la muawa kaburini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Eee Mungu wafungue moyo wanasiasa wenye uwezo wa kumsaidia mtot huyu. Wape uweze wa kujiweka katika maisha ya huyu mtoto.
    Amina.
    Viongozi wetu wengi wanaenda India na wenzao huenda kuwajulia hali yaana kama vile India ni Mbezi na Muhimbili lakini sisi wengine ni kumlilia tu Mingu atume malaika wake!

    ReplyDelete
  2. inshaallah Mungu atamjalia wepesi ,haya matibabu je hayawezi kufanyika Nairobi au AFRIKA YA KUSINI,NA HIZO 6000 US DOLLAR NI PAMOJA NA WANAOMPELEKA NAULI AMA VIPI MAANA KAMA NI HIVO KWA NINI TUSIWASILIANE NA BALOZI WA TZ KULE INDIA AKAMPOKEA YEYE TU NA KAMA WAJITOLEE BAADHI YA WANAFUNZI KUMSAIDIA KULE INDIA ILI KUPUNGUZA HIZI GHARAMA MAANA WATU WATAKATA TAMAA KUONA KIASI NI KIKUBWA KUKIFIKISHA,MAWAZO YANGU TU HAYA

    ReplyDelete
  3. Kwa mfumo wa sasa wanyonge tuchangiane wakubwa wapelekwe India, Afrika ya Kusini na Ulaya kwa matibabu kwa pesa za KODI YA ZETU. La muhimu kwa serikali, VIONGOZI WATIBIWE HAPAHAPA BONGO hapo waboresha mahospitali yetu kwa kuwahudumia watu wote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...