Mkuu wa Kiengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma akizungumza wakati wa Warsha ya siku tatu kwa wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya Kijamii (BLOGS) hapa nchini kuhusu Wizara hiyo inavyoweza kupeleka habari kwa urahisi kwa wananchi wa kawaida iliyofanyia Kibaha mkoani Pwan,hivi karibuni.

Na Othman Michuzi.

Kutokuwa na utamaduni wa kupenda kusoma vitabu, na taarifa mbali mbali zinazohusiana na maendeleo ya nchi imetajwa kuwa ni kikwazo kikubwa katika mawasiliano kati ya wananchi na taasisi mbali mbali za serikali, jambo ambalo ni hatari katika Taifa linaloendelea.

Kwa mujibu wa utafiti usio rasmi uliofanywa na baadhi ya waandishi wa habri za kijamii nchini, ni asilimia tisa tu ya watanzania, ndio wenye utaratibu wa kupenda kusoma, asilimia iliyobakia, hupata habari kwa njia ya kusikia, ama kwenye vyombo vya habari au kwenye maongezi ya kawaida.

Hii ni moja ya taarifa zilizowasilishwa kwenye warsha ya siku tatu iliyoshirikisha baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii na magazeti tando, kwa kushirikiana na Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Fedha, katika kujadili jinsi ya kuboresha mawasiliano kati ya wananchi na taasisi za kimaendeleo ili kurahisisha ufikaji wa taarifa za kimaendeleo kwa wananchi.

Kutokana na tabia hii ya kutopenda kusoma, wananchi wengi wamekuwa wakikosa kujua mambo mengi ya kimaendeleo yanayofanyika nchini kwa sababu taarifa hizi mara nyingi huwekwa katika maandishi.

"Limekuwa ni tatizo kubwa sana hapa nchini, watu hawajui kitu na hawataki kujua kwa sababu hawapendi kusoma", alisema wakati akichangia mada mmoja wa washiriki wa Warsha hiyo,Bw. Josephat Lukaza.

Katika Warsha hiyo ya siku ambayo pia ilihudhuriwa na maafisa habari kutoka sekta mbali mbali za kimaendeleo, wadau walikuwa wakitafuta njia mbadala itakayosababisha wananchi kujua mambo mbalimbali ya kimaendeleo ya nchi ili kujua hali halisi ya uchumi wa nchi inavyoendelea.

Naye Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha Wizara ya fedha, Bi Ingiahedi Mduma, alisema ipo haja ya kuwa wabuhifu katika kuhakikisha kwamba kwa njia yoyote ile, tunahakikisha kwamba wananchi wa kawaida, hasa wa vijijini, wanapata taarifa husika kwa wakati muafaka.

Amesema taarifa za kimaendeleo za nchi ni haki ya kila mwananchi kujua na ndio maana sasa wameamua kukaa chini na kuumiza vichwa katika kutaka kujua jinsi ya kuwafikia asilimia kubwa ya wananchi, mijini na vijijini. 

Warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro Park Hotel, maeneo ya Misugusugu, wilayani Kibaha, mkoa wa Pwani ambapo pia mikakati mbali mbali ya kimaendeleo ilijadiliwa.

Baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (Blogs) wakimsikiliza Mkuu wa Kiengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma (hayupo pichani) wakati wa warsha hiyo ya siku tatu
Baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (Blogs) waliohudhulia Semina hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. wasemaji wa Wizara, Kmapuni kubwa kama TAZARA, TANZANIA RAILWAYS, TANESCO, TANAPA na hata makampuni kama SAID SALIM BAKHRESA SSB, CLOUDS MEDIA N.K siyo blogs tu ndiyo sehemu ya kuwasiliana na jamii ndani na nje ya Tanzania hata YOUTUBE pia ni sehemu ya buree kuwasiliana na jamii.

    Ni jambo la kushangaza mawasiliano ya bure ya youtube taasisi kubwa nilizotaja hapo juu hawapo ila wasanii wa BONGO FLAVA, TAARAB, KIDUKU ndiyo wanaobebe bendera ya Tanzania youtube.

    Watu mbalimbali wamekuwa wakijaribu kupata taarifa mbalimbali kwa mfumo wa buree wa youtube kuhusu shughuli za bandari, usafiri wa majini/anga/barabara/viwanda/ vyuo vya juu vya elimu n.k lakini hakuna ktk youtube bali ni sanaa tu ndiyo wanaongoza.

    Inabidi taasisi hizo mabli ya sanaa na nyie mawizara, kampuni za ummma/ binafsi n.k pia mtujuze kwa youtube mipango yenu, mafanikio yenu n.k.

    Nchi kama Kenya kwenye youtube utakuta habari za kibenki, kielimu, utalii, biashara n.k zilizotengenezwa na wa-Kenya ktk youtube kwa wingi.

    Pia watu kama kina MichuziMedia, HakiNgowi na makampuni mfanye zaidi ya blogs kwa kuingia katika mfumo wa video youtube kutuhabarisha masuala mbalimbali mkishirikiana na makapuni tajwa niliotoa mfano hapo juu na siyo SIASA, JINAI, DINI na SANAA tu.

    Mdau
    Google Youtube

    ReplyDelete
  2. Uvivu wa kusoma ni kikwazo cha mawasiliano na pia maendeleo.

    Watanzania tuna hulka mbaya sana ya uvivu wa kusoma, mfano hata kwenda Maktaba inakuwa ni mgogoro, magazeti hatusomi, ukiona mtu anasoma Kozi ujue pana moja ya haya hapa:

    1.Anatafuta kupandishwa Cheo kazini
    2.Anaogopa kupunguzwa kazini
    3.Anakwepa majukumu Ofisini

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Tue Mar 26, 11:07:00 pm 2013. Mimi ninafanya kazi serikalini na ninafanya shahada ya uzamili na sina moja kati ya hayo uliyotaja ! Hakuna sheria isiyo na mipaka.

    ReplyDelete
  4. Wadau Kusoma ni muhimu kwa maendeleo zaidi kama Madu wa 2 anavyosema.

    Hebu angalia jamii ambayo haizingatii usomaji itakuwa vipi?

    Si itakuwa jamii mbumbumbu?

    ReplyDelete
  5. Mtoa Maoni wa 3 anony wa Wed Mar 27, 01:23:00 am 2013

    Ofisa wa Serikalini, sasa siku zote hizo ulikuwa wapi ndio wende ukasome leo?

    Kama ungekuwa na morale wa kweli wa masomo usingekimbilia kuomba kazi baada ya Shahada ya Kwanza.

    Wewe umeingia Kazini na moja kati ya hayo matatu (3) aliyotaja Mdau ndio yanakufanya unarudi tena darasani.

    Sasa kwa nini ukurupuke kujitetea kama wewe sio mmoja wa hao?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...