Pambano la masumbwi kutetea makanda wa mabara wa WBF(world boxing forum) wategemea kufanyika katika uwanja wa mkwakwani jijini  Tanga kwa  kuwakutanisha  Alan Kamote, ambae ni bingwa mtetezi wa  mkanda huo aliouchukua  nchini Malawi  kwa  kuzipiga na  Jumanne Mohamed  wa tanga  ambae anavyo vigezo  na sifa zote  za kuugombania ubingwa huo.
Jumanne Mohamed ambae alipata nafasi  ya kugombania  ubingwa  wa  dunia  nchini Namibia na kuipoteza kwa kupigwa na mnamibia  nafasi hiyo imejirudia tena,safari hii katika ubingwa wa mabara na kuugombania katika ardhi ya nchini mwake.Muandaaji wa pambano hilo Ally Mwanzoa  akizungumza  na viongozi wa ngumi nchini pamoja na katibu mkuu wa ngumi za kulipwa  Ibrahim  kamwe  amesema ameamua kuandaa pambano hilo ili Alan kamote autetee  mkanda wake alioupata  Blantaya nchini Malawi usije ukapoteza kwa kutokuutetea ubingwa wake huo, na kukaa na uongozi wa ngumi  kwa kuangalia bondia gani anafaa  na ikaamuliwa  jumanne Mohamed anafaa kutokana na sifa alizonazo na upinzani walionao  mabondia hao utaleta mshawasha na msisimko mkoani Tanga, kwa hiyo haina haja ya kumleta mtu kutoka nje ya nchi.mwanzoa aliendelea  kwa kusema pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi  kati jj ngotiko  na  haji juma wa Tanga katika pambano la raund kumi, na kutakuwepo na mapambno mengine mengi y a utangulizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...