Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bw. Yusuf Abdallah ambaye ni mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25, katika wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mhe. Hawa Ghasia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25 Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole kijana Baqir Dhamji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25. Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya MOI.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakimpa pole kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25.PICHA NA IKULU.
Hivi hawa walioumia wanatibiwa na serikali au wanajihudumia wenyewe? Kama ni serikali, mbona wako ward tofauti?
ReplyDeleteWho is responsible for their treatments? Double standard?
Sijui itafikia wapi hatua ya kuwatafuta wahusika waliosababisha kuanguka na kuua ndugu zetu,ila ninachojua na nina uhakika ni kuwa kuna majumba mengine meeengi hayapo katika hali ya kiusalama na sijui kama viongozi wetu wanajua kuwa wanahitajika kuanzia sasa kufanya uchunguzi wa kina kabla ya balaa jingine halijatutokea.Na mwisho sina budi kuelezea kuwa huyu Raisi wetu huwa ananisisimua sana kwa jinsi alivyokuwa simple na mwepesi kuwajulia hali wagonjwa na hali hii inatia moyo sana.Na hapa sina maana kuwa kila anachokifanya nchini ni sahisi ila ukweli ni kuwa ANAJITAHIDI MNO KATIKA UPANDE HUU WA KUWAJULIA HALI WATU WAKE. BRAVO!!!
ReplyDeleteJamani naomba kujua walio fariki watoto wangapi na watu wazima wangapi. Sijaona maelezo ya marehemu naona idadi tu.
ReplyDeleteNawapa pole sana hao wahanga wa hiyo zahma,sasa mzidishe ibada mana msidhani hao wenzetu 26 hawakuwa wajanja au walizembea isipokuwa ni mipango ya Mungu tu
ReplyDeleteanon wa kwanza: nadhani wanajilipia gharama wenyewe kwani naona mtoto wa kiarabu yuko first truck wakati wenzie wako kule kwenye wodi za kajamba nani
ReplyDeleteWhy is there no attention paid to the corrupt system and people who have victimized these innocent workers and children due to their personal greed? They need to be given corporal punishment swiftly - all of them!
ReplyDelete