Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, wanaocheza soka la Kulipwa nchini Congo DRC katika Timu ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu (kushoto) na Mbwana Samatta wakizungumza na mmoja wa mashabiki wa Soka nchini Tanzania aliyewalaki walipo wasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana tayari kwa kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Morocco.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, wanaocheza soka la Kulipwa nchini Congo DRC katika Timu ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu (kushoto) na Mbwana Samatta wakiwa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili tayari kwa kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Morocco Jumapili hii katika mechi ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani.




Jamani hebu tuangalie ni vipi tutawa enzi na kuwafurahisha hawa Vijana wetu Mastaa wa Michezo wakiwa wanakuja nyumbani?
ReplyDeleteKwa nini wasipewe nafasi ya kusafirishiwa kwenye ndege na Ma Benzi yao wanayoendesha huko wanakocheza wakija nchini kulitumikia Taifa?
Sasa, kila usafirishaji wa magari ktk ndege gharama za juu zitozwe na pia tushike Kodi hata kwa hawa wabebaji wa Bendera ya Taifa ?
Hivyo ndivyo tunavyoweza kuwekeza ktk kuwaamsha ari na mwamko wao wa Uzalendo!!!
Pumbalesi hizo pesa za kusafirisha hayo magari. si wapewe watoto yatima hata wao wale vizuri wavae vizuri walale vizuri
Deletemdau wa kwanza usirudie tena kuongea upuuzi kama huo ni hayo tu
ReplyDeleteMdau wa 2 anony wa Tue Mar 19, 09:22:00 pm 2013
ReplyDeleteWewe ndio umetoa Pumbalesi, Fedha ya kulisha yatima na watoto wa mazingira magumu unatakiwa UCHANGE WEWE pamoja na ZILE LA MAFISADI zikamatwe ndio zitolee huduma hizo!
Wewe ufanye wizi Serikalini na Fisadi ahujumu mali ya nchi na Serikali, wewe Mwizi wa mali ya umma na Fisadi mtumie fedha zenu kujengea Mabaa na Pubs halafu Star wa Michezo anayeitumikia nchi vyema asipewe heshima yake?