MWIMBAJI wa muziki wa Injili kutoka Zambia, Ephraim Sekeleti amethibitisha kushiriki tamasha la Pasaka litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Machi 31 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Sekeleti amekubali kushiriki baada ya mashabiki wengi kumpendekeza.



Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu anatamba na albamu mbalimbali zikiwemo Acha Kulia na Mungu Mwenyewe. Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hizo ni Uniongoze na Kidonge cha Yesu. Wasanii wengine ambao tayari wamethibitisha ushiriki wao ni Upendo Nkone na Rose Muhando kwa Tanzania, wakati wan je ya Tanzania ni Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.


Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na  litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.


Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...