Ndugu zangu habari za wikiendi. Yapo mambo machache
ningependa kuwashirikisha ili kuweka kumbukumbu sawa na pia kuzuia upotoshaji
ambao unaweza kujitokeza siku za usoni iwe kwangu, kwako au kwa mtu mwingine.
Mojawapo ya mambo makubwa ambayo yamejitokeza siku za karibuni hasa katika
suala la Teknolojia na habari ni jambo la sheria za faragha (privacy and
privacy lawas). Tumeshuhudia kufungwa kwa gazeti za News of The World, mali ya
bilionea Rupert Murdoch wa Kimarekani baada ya kudhihirika alitumia wataalam wa
teknolojia (hackers) kutafuta siri za watu mashuhuri kwa kuingia katika simu
zao za mkononi kinyume cha utaratibu na sheria za faragha (Privacy Laws).
Tumeshuhudia pia wahalifu hao hao wa mtandao wakifanya mengi kama kuvamia kwa
mitandao ya makampuni makubwa kama Sony na mengineyo na hata katika mitandao
hii ya kijamii upo wakati marafiki zako wanakwambia mbona umenitumia kitu
kisichoeleweka, na baadaye kuja kugundua kwamba si wewe uliyefanya hivyo.
Tarehe 1, 8 na 9 mwezi huu wa Machi nilikuwa Dar es Salaam kwa shughuli zangu za kawaida kimaisha lakini ziko updates 5 zilifanyika hapa moja ikimhusu ndugu Absalom Kibanda. Ni ajabu kwamba baadhi ya waandishi tena waliojivika taji la usahihi katika uandishi waliiandika habari hiyo bila hata kuniuliza kwamba ni nini kinatokea. Tunajitahitahidi na kutamani kuwa na Taifa la waandishi makini na wenye kufuata maadili lakini wapo wanaoturudisha nyuma. Ni ajabu gazeti kuandika jambo lisilo la kweli huku wahusika wakiwa na kila uwezo wa kumfikia yule wanayedhani kwamba ameandika na kumhoji ili kuhakiki habari. Kazi ya uhariri ni kuhakiki. Ikiwa mtu atakimbilia kuandika jambo likuhusulo ambalo hana hakika nalo na alikuwa na kila uwezo wa kuwasiliana na wewe na kukuuliza lazima utajiuliza maswali mengi. Kwanza: Nini hasa lengo lake na pili ufahamu wake wa kile anachokifanya kwa maana ya taaluma yake katika kazi anayoifanya.
Napenda kuwaambia kwamba katika tarehe tarehe hizo mwezi huu wa Machi, wahalifu wa mtandao wakiwa eneo la Njiro na baadaye Kijenge mjini Arusha (Kila post ilionyesha eneo ilipotoka), (wakati huo mimi nikiwa Dar es Salaam) waliingia bila idhini kwa njia haramu (Hacking) katika anuani yangu ya Facebook na ku-post habari hizo tano. Sasa nimeliacha jambo hilo katika vyombo stahiki vya ulinzi na usalama ili kufuatiliwa kadiri ya taratibu zao.
Natoa wito kwa ndugu zangu waandishi kujitahidi kuhakiki habari kabla ya kuzipeleka katika vyombo vyao. Hii itasaidia 1. Wao kujenga heshima mbele ya jamii 2. Kufikisha kile hasa ambacho ni habari 3. Kuzuia mikanganganyiko isiyo ya lazima. Haya yakizingatiwa nadhani hata sintofahamu hizi za uandishi wa habari unaotokana na hisia na vyanzo vumbi na ufahamu mdogo wa jambo utaondoka na tutakuwa na jamii ambayo haki na uwajibikikaji wa wanahabari kwa jamii utaonekana kutendeka
Niombe radhi kwa ndugu yangu, rafiki yangu na pia mwalimu wangu, Ndugu Absalom Kibanda kwa usumbufu wowote uliojitokeza ambao naamini watu wasio na nia njema walitaka kuutumia kuleta hisia tofauti katika jamii na pia kumpa pole kwa mara nyingine tena kwa maumivu yaliyosababishwa na ujangili huo. Namuombea kwa Mungu ampe unafuu mapema zaidi ili arudi katika meza yake kuendeleze harakati za kupambana na mchango wake katika kuleta maendeleo ya kweli kwa nchi yetu. Pili, pole pia kwa wote ambao kwa namna moja au nyengine walikwazwa na uzushi huo, kwa kuwa sina tatizo lolote na Bwana Kibanda na wala nisingependa lililomtokea limtokee yeye wala mtu mwengine yeyote.
Ni imani yangu ya dhati kwamba vyombo husika katika nchi yetu havitasita kulitalifanyia kazi jambo hili na ukweli juu ya nini kimemtokea Bwana Absalom Kibanda utajulikana na kuwekwa bayana.
Mwisho, shukrani kwa wote mlionipigia simu kuhusu hili, tuko pamoja na nawatakia kila la kheri katika shughuli za ujenzi wa Taifa letu hili la Tanzania ambalo msingi wake umejengwa katika haki, umoja, amani na kujali hali za watu wake.
Asanteni sana.
Ndugu yenu,
Ridhiwani Kikwete,
Jumapili Machi 17, 2013.

Pole sana na soo la hackers Kama ni kweli lakini. Facts kadhaa - News of the world newspaper haikufungwa na serikari bali mmiliki wake ndio alieamua kuifunga na kuanzisha The Sun on Sunday ikiwa na wafanyakazi Wengi wale wale wa News of the World. Nimrjifunza kuwa Watanzania akaunti zetu za Facebook na yahoo zikiwa hacked tukaripoti kwa vyombo vya ulinzi na usalama, bila Shaka watafuatilia.
ReplyDeleteAlexbura dar
Cry baby
ReplyDeleteNi sawa ume-acknowledge kuwa account yako ilivamiwa na hackers...inawezekana. Lakini umechelewa sana kukanusha kuwa siyo wewe uliye comment kwenye hiyo issue. Wakati mwingine ni vyema ku-act haraka. Siwezi kusema ni wewe uliyeandika hapo, inawezekana ikawa ni mtu anayekufahamu au ndugu wa karibu ambaye amekariri password yako...Hivyo be careful. Hata hivyo ni vizuri umejitokeza kuondoa utata huo. Huyo aliyeingilia account yako na kutoa comment kama hizo anastahili kuitwa mnyama kwani hana akili za binadamu, hakuna binadamu mwenye akili timamu anayeweza kumkejeli au kutoa maneno yanayotia machungu kwa mtu aliyepoteza sehemu ya mwili, just imagine jicho lako linachomwa na kung'olewa ungejisikiaje? TUWE BINADAMU JAMANI!!
ReplyDeletePole sana Ndugu Ridwiwani!
ReplyDeleteIle tu kwamba wewe ukiwa Jijini Dar Es Salaam na meseji ktk Mitandao ya Jamii zikitumwa kutoka Njiro na Kijenge Arusha,
Moja kwa moja hizo ni habari za uzushi na uchochezi dhidi yako.
hujachelewa kabisa kutoa muelekeo wako. huwezi tu kukurupuka ukaita vyombo vya habari, mwenye busara lazima apime ajue ilikuaje afu atafute ushauri ndio utoe msimamo wako. UKO VERY RIGHT BUT NOT PERFECT, USJALI HIZI NCHI ZETU ZIMEKUA ZA FITINA SANA HUMJUI ALIYESOMA WALA ASIYESOMA, POLE SANA BUT WHAT U DID IS GUD
ReplyDeleteDuh! Too late, why!!!! Jambo hili lilikuwa muhimu sana, ulitakiwa ku-act immediately AU ULIKUWA UNASUBIRI KUANDIKIWA DOGO, HILI KANUSHO??? NILIVYOLISOMA INAONEKANA KAMA UMEANDIKIWA VILE, NA NDIO MAANA KWA STAHILI HII MPAKA WAMEINGIA KWENYE FACEBOOK YAKOO..
ReplyDeleteKUWA MAKINI, IKIWEZEKANA JITOE KWENYE HIYO FACEBOOK.
Nahisi kama unarudia kile kile kilichofanywa na waandishi wa hiyo habari. gazeti unalijua jina na muandishi wa hiyo habari unamjua jina, kwa nini usiwataje kuwa hawa ndio waliohusika ili iwe mfano kwa wengine?
ReplyDeleteDu Ukubwa ni Jalala, Ndg. yanakukuta yote haya kwa nafasi uliyo nayo ndiyo inakuponza!
ReplyDeleteKwanini kila mara usemwe wewe tu?
ReplyDeleteUshauri,
ReplyDeleteKama itawezekana ili kuepeuka mabalaa mengine zaidi Ndg.Ridhiwani ungejitoa ushiriki na matumizi ktk mitandao ya mawasiliano na kuangalia mtindo mpya wa maisha ya kuishi kama uko kwenye Mfumo wa Ujima bila simu wala inteneti!
Toka kwenye face book, utaokoa mengi ikiwepo muda ambao ni mali
ReplyDeletePole sana, ila mti wenye matunda mengi ndio unaopondwa mawe. You are just a victim of circumstances, watu wana chuki sana na wivu kwa failures zao amgazo si wewe ulisababisha. You did a good thing kusubiri na hukukurupuka kama wafanyavyo wengine kisha wanatoa makanusho yasiyo na substance! Pole sana and ask God to be your greatest Protector at all times!
ReplyDeleteUkiwa kama Kada Mwandamizi wa Chama Tawala na ukilinganisha na Ukanda zinakotokea hizo Postings (Njiro na Kijenge-Arusha) mojamoja wa kushikwa hapa wamojawapo ni ktk wana Chadema!
ReplyDeleteLipi jema?
ReplyDeleteKwa nafasi uliyo nayo katika jamii, mengi yatakukuta kama utaendelea kutumia fb ushauri wangu jitoe ili uishi kwa amani kuepuka malumbano ya kila siku na binadamu wasio kuwa na utu.
ReplyDelete