Baadhi ya Wakazi wa jiji la Dar wako kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na magonjwa mbalimbali  milipuko ikiwemo homa ya matumbo,kufuatia kuwa na tabia ya kula kula vyakula ambavyo haviko katika hali/mazingira ya kiafya na salama zaidi,hasa ukizingatia msimu wa mvua umekwishaanza ambao ni rafiki sana kwa magonjwa ya milipuko.Pichani ni baadhi ya wateja wakila vipande vya samaki aina ya pweza,ambavyo vimeachwa wazi pasi kufunikwa ama kuwekwa tahadhali yote yote ya kulinda afya wateja wake,hali ambayo inaweza kusababisha magonjwa ikiwemo homa ya matumbo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Sasa wewe hukuonaChakupigia mfano wa hayo magonjwa ya tumbo zaidi ya chakula tamu Kama hii wewe vipi bwana aa!!!!si wako samaki sangara mbona hujatoa picha yake ??.

    ReplyDelete
  2. Weeee acha za kuleta hizo.Hao pweza ni moto sana wala hawana ugonjwa wowote.Hata babu yako alikula sana hao pweza na aliishi miaka 100.

    Huo ni ujasiria mali vijana wetu hawataki kuishi kwa kuiba.Ni kweli kuweka tahadhari lakini naona tahadhari wanayo.Hata ulaya biashara hizo zipo tembea uone.Vitu hivro ni vyamoto nzi hatuwi.

    ReplyDelete
  3. Unaposema watu waache kula hovyo je unafikiri wanajitakia. Mtu una njaa una vijisenti vyako mfukoni, utakula chochote unachomudu kununua. Binadamu wote tunapenda kula chakula kizuri lakini maandalizi ya chakula kizuri ni gharama ambayo sisi walala hoi hatuiwezi. Yakisha wekwa mazingira ya kiafya bei inakuwa juu. Tunategemea hali ya nchi itabadilika karibuni na sisi tuanze kupeta. Halmashauri za jiji au mji wanajua wakiviondoa hivyo vyakula twafa au beriberi itasimama na sisi. Degelavita.

    ReplyDelete
  4. watu wa bara bwana, kwenu huko hata vyoo hamchimbi hujaona kuwa hilo ni tatizo tena kubwa ki'binadamu na kimazingira, unakuja kuongelea vitu visivyo na madhara kiafa na kimazingira pia...

    ReplyDelete
  5. Pweza ni samaki watamu bwana na hawasababishi vitambi kama chama choma. Wataalam wanaita "white meat". Achana na kampeni zako hizo labda ungemshauri mjasiria mali atafute sanduku la kioo awaweke hao pweza. Itapunguza hatari ya nzi.

    ReplyDelete
  6. Huyo Mpiga picha atakuwa ni Mtani wenu ninyi wa Pwani na samaki wenu Pweza, yeye mtu wa Bara anakula Kambare wake !

    Mmesahau watu wa Pwani kuwa huko Bara mikoani mna watani wenu?

    ReplyDelete
  7. Kinyama cha samaki cha hamu chanitia hamu!

    Ya nini nipite niwaone samaki wamenona, nijivunge kula etu usafi niende nikijilaumu na nikisononeka?

    ReplyDelete
  8. Wewe Mpiga Picha ungetoa ushauri kwa wauzaji ili waboreshe usafi!

    ReplyDelete
  9. Mpiga picha hii wewe mwenyewe ulipata uchu !

    Sema tu ni vile ulikuwa na makoti makoti yako na mikoba ya Laptop begani ukaona aibu kuchukua stick na kudokoa finyango hizo.

    Ulichofanya ni kufungua Mkoba ukatoa Kamera ukapiga picha!, hata wewe ulitaka ule lakini ukajistukia ukaishia kupiga picha tu.

    Unabisha wakati ukipiga picha kona pale ukingoni wa Feri njia ya kuingia kupandia Kivuko cha kwenda Kigamboni nilikuona?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...