Askari wa Usalama Barabarani akipambana na dereva asiyetaka kutii amri halali ya kusimama asubuhi hii katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es salaam...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Well equipped techniques!

    ReplyDelete
  2. Jamani mioyoni mwetu bado tunaugulia na kusikitika kifo cha mwanamke mwenzetu traffick aliekufa akiwa kazini kwa kugongwa na gari....ambapo nia imani kila kitu kinapotokea tunapata fundisho au mafundisho. Kweli huyu traffic alieamua kupanda hii gari anataka nini kifo au ulemavu ni nini hasa. Mbona askari wetu wa barabarani wanakosa hekima jamani wanafanya kazi kama mashine iliyosetiwa. Je zana alizoshika mkononi ni kwa ajili gani urembo au hajui matumizi yake. Kwa nini hachukui maamuzi ya kuandika number ya gari au awe na radio call awasiliane na mwenzie gari wakitaka kulikamata askari hawashindwi.Sasa hapo anaonekana kakosa hekima na wanasahau makosa ya barabarani kulipa fine ni kwa sana tuu. Kweli anahatarisha uzima wake kwa maamuzi ya kibabe. Hebu jeshi la police liamue kufanya some trainings to build capacity za watendaji wake wa barabarani. Yote haya yanawakuta kwa sababu ya maamuzi yao ya ubabe kukaa mbele ya gari na kama ivi kupanda gari. Je driver akiamua kureverse then akamdondosha akamkanyaga itakuwaje.

    ReplyDelete
  3. Tamaa ya pesa tu hio....

    ReplyDelete
  4. hana lolote huyo trafic anatafuta umaarufu tu!

    ReplyDelete
  5. we muache ajui sisi kama hatuna mda wakulia tena!

    ReplyDelete
  6. Mungu anasema "Tazama watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"

    ReplyDelete
  7. Ndugu zangu Wazalendo, hii ni hatari kwa maisha ya huyu mtumishi wa serikali. Kalamu yake ni kuandika namba za madreva wasiojua kutii bila shuruti. Wajeuri wapo, lakini mchukulie kwa ustaarabu hata kama dreva sio msitaarabu. Andika namba kisha rusha hewani, atasimamishwa mbele ya safari au siku nyingine tuu.

    ReplyDelete
  8. napenda mentality za askari wetu pamoja na wanajeshi wetu. woote wanaamini kuwa wanaogopwa na kuhushimiwa saaaana wanapokuwa na magwanda yao kiasi kuwa wanahatarisha maisha yao kiasi hiki.

    Huyo trafu iki kafanya hayo kwa sababu tu anaamini akimshika huyo dereva atamshitaki zaidi kwa kutoheshimu vazi la polisi amesahau kabisa kuwa kwa kujiweka mbele hapo amehatarisha maisha uka yake. Amesahau kabisa kama nchi hii imejaa vichaa wa kila aina.

    ReplyDelete
  9. Yaani hata wiki haijaisha tangu yule traffic apoteze uhai akiwa kazini, huyu naye anakuja na staili hii? Kweli sikio la kufa halisikii dawa.

    ReplyDelete
  10. Mama mbavu zangu.... eeeeh! Natamani ningekuwepo live nione mkanda mpaka mwisho. Mdau ilikuwaje hatima ya mambo?

    ReplyDelete
  11. Kwanza inatakiwa ashtakiwe anahatarisha usalama wa dereva, watumiaji wengine wa barabara na wake pia.

    ReplyDelete
  12. Njaa tu zinawasumbuia..hapa anatafuta mshiko tu hakuna cha utii wa sheria wala nini...hebu cheki alivyochoka

    ReplyDelete
  13. Nakufa kwa kicheko jamani. Kweli wonders shall never cease.

    ReplyDelete
  14. He is doing his job at whatever expense Ajalini kazini ipo.

    ReplyDelete
  15. Huyo trafik hana lolote ameomba lift kiaina,na akiendelea mauti yanamngoja!

    ReplyDelete
  16. Na technologia yote bado askari anakimbizana na gari? Redio wanazo, simu wanazo, kamera wanazo, etc. Huu ni umasikini wa kufikiria au ni u-bishoo?

    ReplyDelete
  17. daah, halafu hapo ukute dereva alitaka kupaki vizuri jamaa akaamua kudanda kabisa. agongwe afu aseme mtu alikataa kutii amri!!

    ReplyDelete
  18. Only Bongo has this upuuzi. Akili maji kabisa.

    ReplyDelete
  19. USHAHIDI NDIO HUO WA MAREHEM ALIE KUFA SIO KOSA LAO ASKARI BALI WANAPO PANGIWA SEHEMU NA WA KUU WAO HIZO SEHEMU ZINA ELEWEKA KIPATO CHAKE KWA SIKU HIVYO LAZIMA KWA SIKU AMPELEKEE AFANDE KIASI FULANI BILA YA HIVYO HATO PANGIWA KAZI NA KUHATARISHA ATOLEWE UTRAFIC RUSHWA TUPU INA NUKA UTAKUTA HATA AKIWA OFF JUMAPILI HAYUPO KAZINI ANA VAA GWANDA NA KUMUAMBIA MKEWE WEKA CHUNGU CHA UGALI JIKONI AKI RUDI UTAMUONA NA MBOGA

    ReplyDelete
  20. Kheeee kila mtu ale ofisini kwake isiwe tabu.
    Good job officer.

    ReplyDelete
  21. Mmh!Hiki kioja kimekaa dezaini ya 'Mazishi saa nane'

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...