Silaha zaina hii na nyingineza zikiwamo ndogo na nyepesi zimekuwa zikisababisha madhara makubwa kwa maisha ya watu wasio na hatia pamoja na ubaribifu wa mali zao. takwimu zinaonyesha kwamba watu zaidi ya nusu milioni hufa kila mwaka ikiwa ni pamoja na wanawake 66,000 na wasichana kutokana na matumizi mabaya ya silaha. Aidha kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya silaha, takwimu zinaonyesha kwamba kati ya mwaka 2000 na 2010, karibu wafanyakazi 800 wa misaada waliuawa katika mashambulizi huku wengine 689 walijeruhiwa
Na Mwandishi Maalum
Macho na Masikio ya Dunia yameelekezwa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ( UM) ambako zaidi wa wajumbe 2000 kutoka mataifa 193 wanakutana katika kile kinachoitwa mkutano wa mwisho kuhusu Mkataba wa Kimataifa wa kudhibiti Biashara ya Silaha ( ATT).
Mkutano huu umeanza siku ya jumatatu kwa kufunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Akiwazungumza wajumbe hao, Mkuu huyo wa UM, pamoja na mambo mengine ameeleza kwamba kama jumuiya ya kimataifa imeweza kuweka viwango vya kimataifa vinavyodhibiti utengenezaji wa T-shirt, midoli na uzalishaji na uuzaji wa nyanya kwanini ishindikane kudhibiti na kuweka viwango kwenye silaha.
Akasema Ban Ki Moon “ Tumeweka viwako karibu katika kila bidhaa kuanzia utengenezaji wa T-shirt, midoli hadi kwenye nyanya, lakini si biashara ya silaha” akahoji Ban Ki Moon
Na kwa sababu hiyo amewataka washiriki wa mkutano huu kuonyesha dhamira ya kisiasa ya kukamilisha majadiliano ili hatimaye ifikapo Marchi 28 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya mkutano watoke na Mkataba, kama ilivyoainishwa kwenye mkutano wa tisa kwamba mkutano huu ni wa mwisho.
Akaenda mbali zaidi kwa kuwahadharisha wajumbe kwamba wanapokutana katika mkutano huu, hawaanzi upya majadiliano ya mkataba, majadiliano ambayo yalifanyika tangu mwaka 2006 wakati mchako wa ATT ulipoanza. Bali wanakuta kukamilisha kazi ya kutoka na Mkataba.
BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI
BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...