Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kanda ya Ilala, Evans Musiba (Aliyesimama), akizungumza Kwenye shule ya Kigilagila ambayo PPF wana watoto waowasomesha kupitia Fao la elimu.Vilevile PPF walitoa Msaada wa Vitabu kwenye shule hiyo.PPF husomesha watoto wa Mwanachama aliyefariki kuanzia chekechea mpaka kidato cha nne.Kushoto ni Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe.Jerry Slaa ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi na Kulia ni meneja wa Pensheni, Bi. Chevu Sepeku.
Meya wa Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam, Mhe.Jerry Slaa, akihutubia wakati wa kampeni ya kutangaza fao la elimu kwenye Kanda ya Ilala.Fao la elimu hutolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF. Katika hotuba yake, Mhe.Meya aliupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kuona umuhimu wa kuwa na fao la elimu kwani fao hilo linamnufaisha mtoto wa mwanachama aliyefariki akiwa katika ajira na kuchangia miaka mitatu au zaidi na hivyo kumuwezesha mtoto wa mwanachama kuendelee kupata haki yake ya elimu licha ya kumpoteza mzazi wake.
Meya wa Manispaa ya Ilala,Mhe. Jerry Slaa, akigawa zawadi kwa mwanafunzi wa darasa la nne, shule ya msingi Kigilagila jijini Dar es Salaam, Ummy Abdallah, wakati wa kampeni ya kutangaza Fao la Elimu kwenye Kanda ya Ilala, shuleni hapo. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Verian Mfugale. Katika hotuba yake ya uzinduzi, Mhe. Meya Slaa aliupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kuona umuhimu wa kuwa na fao la elimu .Ummy ni mmoja wa wanafunzi wanaofaidika na fao la Elimu na Mfuko wa PPF.
Meya wa Manispaa ya Ilala akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Msingi Kigilagila.
Meneja wa Kanda ya Ilala, Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Evans Musiba, akigawa vitabu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kigilagila iliyoko wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...