Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua kwa kipindi kingine Balozi Christopher
Liundi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa-Arusha
(AICC).
Aidha, kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe (Mb.)
amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kama ifuatavyo:-
1.
Bw. Aggrey Mlimuka
2.
Bw. Dash-Hood Mndeme
3.
Dkt. Ali Mndali
4.
Mhe. Balozi Abdi Mshangama (Mstaafu)
5.
Mhe. Faith Mtambo (Mbunge wa Viti Maalum)
6.
Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala (Mbunge wa Nzega)
7.
Mhe. Mary Chatanda (Mbunge wa Viti Maalum)
8.
Mhe. Ali Mzee Ali, (Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi - Zanzibar)
9.
Bw. Wilson Masilingi (Mbunge Mstaafu)
Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni kwa
kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 06 Machi, 2013.
IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE
NA
USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM
8 MACHI, 2013
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...