Na Anna Nkinda – Maelezo, Mwanza
Imeelezwa kuwa kutokana na tatizo la baadhi ya kina mama wajawazito kuchelewa kufika Hospitali mapema kujifungua wengi wao wanakufa kutokana na tatizo la kupasuka kwa mfuko wa uzazi, kutokwa na damu nyingi kabla na baada ya kujifungua na kifafa cha mimba.
Hayo yamesemwa jana na Daktari wa Mkoa wa Mwanza Dk. Valentino Bangi wakati akisoma taarifa ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza - Sekou Toure kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyefika Hospitalini hapo kwa ajili ya kufungua mradi wa kisima cha maji uliojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti.
Dk. Bangi alisema kuwa tatizo la vifo vya kina mama wajawazito na watoto limepungua kwa kiasi kikubwa katika Hospitali hiyo ukilinganisha na miaka ya nyuma kwani mwaka 2012 vifo vilivyotokana na tatizo la uzazi vilikuwa 10 ukilinganisha na mwaka 2011 ambapo kulikuwa na vifo 15.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...