Mkuu wa Vodacom kanda ya kaskazini Bw. Philemon Chacha akigawa vifaa vya shule  kwa baadhi ya watoto wenye ulemavu wa akili wa kituo cha KKKT usharika wa Longuo Mjini Moshi  ikiwa ni sehemu ya zawadi mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini vyenye thamani ya shilingi Milioni  1.5 ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Pamoja na Vodacom.

 Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili cha KKKT usharika wa Longuo Mjini Moshi  walipotembela kituoni hapo na kukabidhi  msaada  wa vyakula, vifaa vya shule na vitu vingine mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 1.5 katika kituo hicho ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Pamoja na Vodacom.

Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Philemon Chacha akifuatilia kwa karibu mtoto mwenye ulemavu wa akili Arnold Justine anavyoandika jina lake kwa ufasaha huku mtoto mwenzie Gloria Isaack nae akishuhudia. Wafanyakazi wa Vodacom kanda ya Kaskazini walitembelea kituo hicho na kukabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi Milioni Moja na Nusu ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Pamoja na Vodacom inayosaidia makundi yenye mahitaji maalum.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...