Pichani kati ni Mwanamuziki nguli wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Sipho Makhabane alipowasili usiku wa jana kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na baadhi ya wanamuziki wenzake (hawapo pichani),tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31,kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama.
Mwanamuziki nguli wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Sipho Makhabane akizungumza na Wanahabari wa vyombo mbalimbali mara alipowasili usiku wa jana kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na baadhi ya wanamuziki wenzake (hawapo pichani),tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31
Mwanamuziki Sipho Makhabane akibadilishana mawazo na Mwanamuziki mwenzake wa nyimbo za Kiroho hapa nchini,Upendo Kilahiro,mara baada ya kuwasilia usiku wa jana kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanamuziki wa kiroho wa kwaya ya Ambassadors of Christ ‘Kwetu
Pazuri’ la Kigali, Rwanda wakizungumza na baadhi ya Wanahabari wa vyombo mbalimbali mara walipowasili mapema jana jioni kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31,ambapo pia watazindua albamu yao mpya itakayoitwa Mtegemee Yesu yenye nyimbo kama vile Kaeni Macho, Mungu Wangu, Tugireurukundo, Ewe Ndugu, Tuombeane, Umwamini Yesu, Msalaba, Twawona, Okuswala na Huruma.
Baadhi ya Wanamuziki wa nyimbo za kiroho wa kwaya ya Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda wakiwasili mapema jana jioni kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31
Mwanamuziki Ephraim Sekeleti wa Zambia ambaye pia aliwasili jana kwa ajili ya kutumbuiza tamasha la Pasaka.Tamasha la Pasaka litafanyika kwenye uwanja wa Taifa jijni Dar es Salaam kesho na litaendelea
Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora
Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja
wa CCM Kirumba, Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...