Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt muda mfupi baaday kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jioni hii
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt wakipokea heshima za nyimbo za Taifa pamoja na saluti ya mizinga 21  katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt na mwenyeji wake wakifurahia burudani mbalimbali
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akipkea shada l maua
Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akisalimiana na kinamama waliofurika uwanjani kumlaki. Picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Makamu wa Raisi au waziri mkuu wako wapi hadi Raisi aende kupokea waziri mkuu wa nchi nyingine?

    ReplyDelete
  2. Huyu ndie mtendaji Mkuu wa serikali ni equivalent na Rais maana wao hawana rais ni ufalme!

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Kwanza Itifaki imetumika inavyostahili.

    Nchi hizi hapa ni mfano wa ambazo Waziri Mkuu ndio mtendaji Mkuu wa Serikali:

    1.Uingereza,
    2.Italy,
    3.Uholanzi,
    4.Japan,
    5.Denmark,
    6.Canada,
    7.Israel,

    Zaidi ya hapo pana nchi zingine ambazo Mtendaji Mkuu Serikali wa sio Waziri Mkuu wala Raisi ni Chancellor kama Ujerumani.

    ReplyDelete
  4. Haya Wanawake Tanzania mmeona hiyo?

    ReplyDelete
  5. Waziri Mkuu wa Denmark ni MKUU wa serikali. Hawana Raisi na mkuu wa nchi ni Malkia (Queen Margrethe II)lakini hana serikali kama Malkia wa Uingereza. Serikali inaendeshwa na Waziri Mkuu.

    Kabla ya kuropoka ujinga, tujaribu kutumia "google" ina majibu yoye, sio lazima uende shule kupata majibu yote. Na serikali yetu kwa vyovyote wana maofisa wa Protocol na wanajua wanafanya nini na wamtume nani kupokea wageni.

    ReplyDelete
  6. Wenzetu wa Denmark Waziri mkuu ndiye kiongozi mkuu wa serikali kwa hiyo ni sahihi kupokewa na kiongozi mkuu mwenzake.

    ReplyDelete
  7. Ingawa Malkia ktk nadharia Malkia ni Head of State, Waziri mkuu ndo mwendeshaji wa masuala yote Denmark pamoja na kutangaza vita. Kwa hiyo huyo ndo haswa counterpart wa JK

    ReplyDelete
  8. we mdau wa kwanza hemu wacha maneno mengi, kumbuka huyu ni waziri mkuu kwenye nchi ambayo haina raisi bali ni nchi ya kifalme, so waziri mkuu kule ana hadhi kubwa kama ya rais. Isitoshe kumbuka nchi inayoongelewa hapa ni Denmark moja ya nchi inayotoa misaada mingi kwa Tanzania na kushirikiana kwenye mengi sana na Tanzania, wacha Rais wetu naye aonyeshe ubinadamu kumpokea mwenzao.Mwisho naomba ujue kuwa Denmark sio masaa mawili kwa Abood kama vile Morogoro, huyu mama ametokea mbali, umesahau maadili yetu ya kupenda na kuheshimu wageni? tena mgeni aliyevuka milima na mabonde. Next time uwe unafikiri kwanza kabla hujaandika.

    ReplyDelete
  9. wewe usmwambie kama mwenzio anaeopoka kaka wewe ulivyo mwelewesha si kaelewa kaka,alikuwa hajui kuwa Denmark wanatumia mfumo gani wa utawala ,hatuwezi kueleweshana kwa hasira mkuu.busara haipatikani kwa staili hiyo au wewe subira huwa huna kaka.wewe huwezi kuwa kiongozi hata wa familia,mtoto akikosa kitu humwelekezi unamwambia aende google .

    ReplyDelete
  10. ingawa kuuliza si ujinga ln mdau wa kwanza nawe, kha!!

    itifaki imezingatiwa bwana... serikali yetu inajua nini inafanya. Majibu yote umeyapata mdau wa kwanza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...