Na Abdulaziz video,Lindi
Baraza kuu la Waislam Mkoa wa Lindi limetoa msaada wa Vifaa vya Ujenzi kwa ajili ya kuunga jitihada za waislamu wa Kata ya Nachingwea na Jamhuri,Manispaa ya Lindi baada ya kujitolea kuchangia ujenzi huo ili
kuimarisha elimu ya Dini.
 Vifaa hivyo ikiwemo Bati,saruji,rangi na gjharama za ufundi vyenye thamani ya Tshs Milioni 2 laki tatu(2,300,000/) vimekabidhiwa na Katibu wa Bakwata mkoa,Alhaj Abdillah Salum kwa maalim wa Madrasa hiyo ya Al Rijala Musalam,Ustadh Abdulwahab Manzi.
 Akikabidhi Vifaa hivyo,Alhaj Abdillah aliwataka waislamu mkoani humo kujitoa na kuchangia ukuaji wa elimu ya Dini ya Kiislam kwa vijana na watoto ili wakue katika maadili yaliyo mema.
'' Waislam tujitoe kushangia elimu hii kwa muskabali wa maisha yajayo mambo mengi yanatokea kutokana na jamii nyingi kutofuata maadili na mafundisho ya dini ni lazima tuamke na tushikamane katika ibada kuombea Nchi yetu Amani''alisema Alhaj.
 Sambamba na msaada huo pia aliiomba serikali kurudisha na kutenga katika mipango yake ya elimu kwa kutoa fursa kwa elimu ya dini kufundishwa mashuleni kutokana na muda mchache anaopata mtoto katika kupata elimu ya Dini kwa siku za jumamosi na jumapili.
 Akipokea msaada huo Ustadh Abdulwahab Manzi aliishukuru Baraza hilo baada ya kuona juhudi za waislam kuchangia ujenzi huo ambapo alibainisha kuwa msaada huo utakamilisha kazi ya Ujenzi huo huku
akitoa wito kwa waislamu wengine nchini ambao wamejaliwa kupata uwezo kuimarisha elimu ya Dini ikiwa pamoja na kujitolea kuchangia madrasa pamoja na Misikiti ili Waumini wapate fursa ya kusoma na kuabudu
 Katibu wa Baraza kuu la waislamu mkoa wa Lindi,Alhaj Abdillah Salum akikabidhi msaada wa kumalizia ujenzi  wa Madrasat Al Rijala Musalam kwa Maalim wa chuo Hicho,Ustaadh Abdulwahab Manzi 
katika eneo la ujenzi Manispaa ya Lindi

Madrasat Al Rijal ikiwa katika hatua za ujenzi na kazi itakamilika baada ya kutolewa msaada na Baraza kuu la waislam mkoa wa Lindi 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mtu ambae hutowa mali yake kwa ajili ya kujitakasa na hali ya kuwa hakuna yeyote aliyemfanyia ihsani ili awe anamlipa isipokuwa anafanya kwa kutaka radhi za mola wake Mkutufu basi atapata la kumrizisha hii ni aya katika quran inayosema kama ifuatavyo Miniimati tujiza ilabtikha ...... inaendela na kumalizikia walasaufa yaridha. sasa leo unapotowa katika hali kama hiyo tuionayo unategemea nini ?
    From Toufiq mchambawima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...