Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia) akiwa na mshtakiwa mwenzake Saleh Mkadamu wakielekea  kupanda basi la magereza baada ya hukumu ya kesi yao ya uchochezi kuahirishwa hadi Mei 9. Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wanakabiriwa na makosa matano ya kula njama na kuingia kwa jinai katika uwanja namba 311/3/4 kitalu T uliopo Markaz Chang'ombe na wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Shs milioni 59 mali ya kampuni ya Agritanza.
 Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akipanda basi la magereza.
 Askari wakiimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakati hukumu ya kesi yake ilipoahirishwa leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Picha ya mwisho inanishangaza sana, wanashangilia nini wakati jamaa 'mvua' imemkaribia? na inalekea hawana kazi hawa na ni kawaida ya vijana wa dini hii kuwa wavivu na kupenda kuonea wenzao wivu wa kijinga wanaochapa kazi

    ReplyDelete
  2. Acha ufala anonymous wa kwanza hapo. ALiyekwambia wanashangilia nani? Hapo imepigwa Takbiir na watu wanaitikia Allahu Akbar. Ina maana kubwa katika dini hii. Kama hujui bora unyamaze, usilete Udini.

    ReplyDelete
  3. Wanamshangilia ndugu yao, mpendwa wao.
    Wewe mwenye dini ya vijana waliokuwa na kazi, wasiokuwa wavivu na wanaochapa kazi, umejaaliwa na Mwenyezi Mungu na hayo hayakuja kwa uwezo wako bali Mungu ndio amekuwezesha. Mungu aliyewafanya hawa washindwe ndiye aliyekufanya wewe uweze. HAYO NI MAPENZI YA MUNGU. Kipofu hakupenda awe kipofu bali Mungu alipanga awe kipofu na hata wewe uliye na macho unaona Mwenyezi Mungu akiamua uwe kipofu unakuwa bila ya pingamizi. Hujaona watu wamezaliwa na miguu miwili wamepata ajali mmoja umekatwa au yote miwili imekatwa?!

    ReplyDelete
  4. Wewe anony wa kwanza kwanini mnapenda sana udini. Unamaanisha nini kusema Vijana wa dini hii kuwa wavivu na kupenda kuonea wenzao wivu wa kijinga wanaochapa kazi? Hebu acha uchochezi na fanya kazi yako inayokuweka mjini. Haya ya udini yaache kama yalivyo. Hao unaowasema wavivu ndio waliomfanya baba yako akaishi kwa amani na kukuzaa wewe. Tafakari kabla ya kuandika upuuzi wako. Hao "unaowaita wavivu ndio walioleta Uhuru wa nchi hii. Fuatilia historia na sio kudandia gari kwa mbele

    ReplyDelete
  5. Acha chuki zako za kidini. Huu ni utamaduni na upendo uliojengeka kwa WaTZ kupena moyo. Hata katika ulingo wa siasa tuliona jinsi wafuasi wa Lema na mungulu walivyosapotiwa mpaka dakika ya mwisho.

    jee siku ngoma ikila kwako hutafika mahakamani na kusaport kwa kumtia moyo mpendwa wako? Unapepo wewe yafaa upepewe.

    kuna vijana lukuki wa dini yako wakiendelea kuingia Dar mjii wa waislamu asli na kujiingiza katika vigenge vya ujambazi, uporaji, ubakaji, biashara ya unga na uhuni kisa.

    mwisho kuwa mstarabu na muungwana kwani dini yako inafunza upendo kama za wengine.

    ReplyDelete
  6. Sio wote watoao maoni wanao-ongozwa na busara. Inabidi kuwasamehe hao.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa kwanza hapo juu nakupa pole, UMESHAMBULIWA mpaka naona raha. Na usithubutu kujibu, ukijibu MASHAMBULIZI mengine yanakuja, hili limekuwa somo kwako siku nyingine utajua nini maana ya UDINI.

    ReplyDelete
  8. Mdau wa kwanza yuko sahihi jamani, hivi Mungu anapenda watu wavivu wasiopenda kufanya kazi wakati ni wazima wa afya? muda wote wapo vijiweni kupiga majungu badala ya kufanya kazi za kuwapa kipatao.

    Wakiambiwa leo tuandamane haoooo wapo njiani harta sababu hawajui unafikiri waqngekuwa na kazi wangefanya haya? Fungueni akili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...