Katika kazi yangu ya kufundisha kuimba, nimekutana na waimbaji wengi hapa bongo ambao hapo awali, kabla ya kukutana na mimi, walikua wana desturi ya kujifunza kuimba kwa kupiga makelele. Nimepata ripoti ya kua kuna baadhi ya kwaya ambazo hushauri wanakwaya wao kupiga kelele hadi siku ifuatayo wanakuta sauti zimakauka. Nimepata ripoti kuhusiana na vijana wa bongo flava wanavokwenda kwenye ufukwe wa bahari kufanya mazoezi ya kuimba kwa kupiga makelele. Sii makosa yao. Kwani asiejue atafanya lolote lile analoambiwa kwa kuamini kwamba hicho kitendo kitamsaidia kua muimbaji mzuri zaidi. Hivyo ndivo jinsi wanaadamu tulivo. 

Kwa mantik hiyo basi, ningependa kutoa ushauri wangu hapa, kwamba huo mwenendo potovu husababisha uharibifu wa sauti, na usipoangalia, unaweza ukawacha kuimba kabisa kwasababu kunakiwango cha uharibifu ambacho hakiwezi kurekebishika. Kwa maana ukisha fikia kiwango hicho, sahau habari za kuimba. Hutakua na sauti tena.

Ni hivi: Sauti, ili kuendana na muziki wenye mpangilio maalum kupitia kinanda, guitar na kadhalika, inatakiwa kuweza kupanda na kushuka kirahisi na bila kelele za kuumiza koo. Na vilevile, hupaswa kua na melodi yakuvutia ambayo inaendana na muziki huo. Sasa basi, ili kuweza kufika katika levo hiyo inabidi ujifunze kuimba kufuatana na fungua (ama key) za muziki kupitia, kwanza kabisa, chombo asilia cha muziki kijulikanacho kama kinanda. Kindanda kina panga sauti yako katika njia tofauti kupitia mazoezi maalum kwa ajili hiyo, kama vile arpeggios, octaves, chromatic scales, descending scales na kadhalika. Hiyo ndio misingi ya kuimba ambayo nimepangilia mazoezi kamili kwenye CD yangu Jifunze Kuimba na Joett. Kama ungependa nikupe assessment ya sauti yako, tafadhali wasiliana na mimi. Assessment za nusu saa hufanyika katika studio yangu siku za Alhamisi, na ni bure kabisa.

Wewe ndio chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!
JOETT
Vocal Coach & Author
Letters from a Vocal Coach

Download Joett tracks from iTunesAmazon MP3TuneCore.
Buy Joett CDs from A Novel Idea Bookstores Dar, Zanzibar, Arusha.
Nationwide CD distribution via Joett Music (Airtel Money, TIGO Money, M-Pesa).
Follow me on Twitter
Become a fan on Facebook  
Follow Joett On Facebook  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Asante sana kwa ushauri, sasa tunakupataje?? Studio yako iko wapi??? una simu au anuani ya baruapepe tunaweza kukuandikia??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...