Dereva wa Bodaboda akiwa amepakia abiria pamoja na Mizigo yake kwa mtindo wa aina yake huku akiwa hana kifaa chochote cha kulinda usalama wake,kama alivyonaswa na Kamera ya Globu ya Jamii,leo katikati ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. michuzi bin mitori hii blogu ni yetu sote tunataka uweke mapicha ya kumwaga ya mashetani wekundu he he heeee.... najua unaona dongeeeee kama vipi hamia manuuu hutopata bp, kisukari, kichumvi, wala total manuuu daimaaaaa. hongereni wadau woote wa manchester united ulimwenguni kote hadi huko mars!

    ReplyDelete
  2. Waguse uone cha moto, hao ndio wenye nchi bwana au hujaona action zao nini? Hao ni moto wa kutoea mbali kama hujui

    ReplyDelete
  3. NA wani jeusi kapiga, wakipata aksidenti wanalaumu serikali ya CCM kweli tuna safari ndefu watanzania

    ReplyDelete
  4. Utafutaji huo fedha kwa mshike mshike wa Bodaboda ,Msela anapata salio lake halafu wewe Mbwiga unamzima mshiko wake!

    Lohhh si atakufa na wewe?

    ReplyDelete
  5. Bodaboda sarafu wanaitafuta kwa bidii sio mchezo!

    Pana siku nilikuwa ndani ya Teksi kukawa na foleni ndefu, pia ktk foleni mstari mmoja palikua na gari lenye matairi makubwa sana zaidi ya yale ya Trekta huku uvunguni kukawa na uwazi mkubwa ambao kama mtu sio mwoga anaweza kupita bila tabu.

    Sasa cha ajabu akatokea Bodaboda na abiria wake nyuma, ktk hali ya ajabu Dereva wa bodaboda akawa anachungulia uvunguni mwa lile gari lenye matairi makubwa akaanza kuminya mafuta aongeze mwendo ili avuke!!!,,,,ohhh abiria wake akampiga makofi ya mgongoni ndio jamaa anazinduka na akasitisha zoezi la kuvuka foleni kupitia uvunguni!

    Hio ndio akili ya haraka ya Madereva wa Bodaboda!

    ReplyDelete
  6. Hii inahatarisha maisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...