Asasi ya Kijamii ya Catherine Foundation jana imetembelea kituo cha kulelea wa watoto cha Matumaini Village kilichopo mkoani Dodoma ambapo walikwenda kutoa misaada mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wa Asasi hiyo, Catherine Magige.
Katika Hafla hiyo Mgeni Rasmi alikuwa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda ambapo asasi hiyo ilitoa vitu mbalimbali vikiwemo, Madaftari, Mafuta, Sabuni, Juice, miswaki na dawa zake, mchele, sukari, nguo za watoto, kanga za wakinadada wanaowalea watoto hao na vingine vingi.
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige akihutubia katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye Kito cha Matumaini Village kilichopo Dodoma alipokwenda kutoa msaada. Kushoto kwake ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda
Mhe Catherine Magige akicheza na mmoja wa watoto wa kituo hicho
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige akiwa na mtoto mchanga anaye lelewa katika Kituo cha Matumaini Village mjini Dodoma jana.
Misaada mbalimbali ikitolewa
jamani chonde chonde na hiyo mikorogo naona sasahivi imerudi kwa kasi sana mikorogo uzalisha kansa punguzeni mikorogo bakieni na rangi zenu asilia za kimatumbi.
ReplyDeleteTafadhali tufike mahali tuziheshimu haki za wasiojiweza kwa kuacha kupiga nao picha tunapowapelekea mitumba au achakula. Sisi majumbani mwetu tukiwapa wanetu vyakula na ngu hatupigi picha na kuzileta magazetitini. The acts of charity should remain between us and the helped group. It is for strengthening our relationship with the God who is the giver and not for show off to the other world.Blessed are those who give without any expectations of being praised.
ReplyDelete