Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwahutubia mamia ya wananchi
waliohudhuria kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo nchini
iliyofanyika kitaifa huko Mlandizi , Mkoani Pwani tarehe 22.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpatia chanjo ya motto Haula Mlondwa
,miezi 6, kutoka katika kijiji cha Vigwaza, wilayani Kibaha, ikiwa ni uzinduzi
rasmi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyoadhimishwa huko Mlandizi tarehe 22.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akinamama na akina baba
waliowaleta watoto wao kwa ajili ya chanjo wakati wa uzinduzi rasmi wa wiki ya
chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi, wilayani Kibaha tarehe 22.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahi na
mtoto Haula Mlondwa, mwenye umri wa miezi
6 ambaye aliletwa kwenye sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa
huko Mlandizi, katika wilaya ya Kibaha, na baba yake mzazi Bwana Mlondwa Omar ,
mkazi wa Vigwaza. Mama Salma alikuwa
mgeni rasmi katika uzinduzi huo tarehe 22.4.2013. Bwana Mlondwa Omar alikuwa ni miongozi mwa
wanaume wawili tu walioweza kuwaleta watoto wadogo kwenye chanjo wakiambatana
na wake zao.
Mke wa Rais Mama
Salma Kikweteakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa maabara wa kituo cha afya
cha Mlandizi ,wilayani Kibaha katika mkoa wa Pwani, Bwana Sostenes Nyang’olo, jinsi ya kuchukua vipimo vya damu
na makohozi kutoka kwa wagonjwa wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa
iliyofanyika huko Mlandizi tarehe 22.4.2013.
Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete akifuatana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa
Dr. Seif Rashid wakishiriki kuimba na kikundi cha kwaya cha Anglican Compassion
kutoka Bagamoyo wakati wa uzinduzi rasmi wa chanjo kitaifa ulifanyika katika
kijiji cha Mlandizi tarehe 22.4.2013.
Viongozi, wageni na wananchi
mbalimbali waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa
kwa watoto wenye umri wa chini ya mwaka mmoja iliyofanyika katika uwanja wa
shule ya Msingi Mtongani iliyoko Mlandizi katika wilaya ya Kibaha tarehe
22.4.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
Mpiga picha John Lukuwi tunaomba maelezo sahihi ya picha.
ReplyDelete