Mbunge Mwidau akikabidhi mifuko kumi ya saruji kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Msambweni Bahati Marungu kwa ajili ya ujenzi shule ya Sekondari ya Kata ya Msambweni.

Mbunge Mwidau akisalimia na wanawake wa kikundi cha wajasiriamali wafugaji wa kuku wa Kata ya Pongwe kijiji cha Marizara.
Mbunge Mwidau, akisalimia na wanawake wa Kata ya Mafuriko, ambao walifika kumlaki katika ziara yake ya Wilaya ya Tanga.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), akipata maelezo ya mradi wa kisima cha maji kutoka kwa Diwani wa Kata ya Mwera Maisha Mkaidi (CUF), wengine ni baadhi ya viongozi na wananchi wa kata hiyo.

MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), awametaka wananchi wa mkoa wake kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Kauli hiyo aliitoa kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza katika ziara yake hiyo katika kata za halmashauri ya jiji la Tanga na Wilaya ya Pangani, ambapo alisema ni muhimu kwa kila mwanajamii kutambua wajibu wake.

“Suala la amaendeleo halina itikadi na sasa sio wakati wa kampeni za uchaguzi, ni jukumu letu kwa viongozi wa Mkoa wa Tanga, kuhakikisha tunashiriki katika miradi ya maendeleo kwa dhati.

“Ni wazi Mkoa wa Tanga tuna kila sababu ya kuhakikisha tunaimarisha uchumi wetu hasa baada ya miaka kadhaa viwanda vyake kufa kutokana na kutokuwepo na usimamizi mzuri. Ikiwa kila mtu atatambua wajibu wake ni wazi tutafanikiwa kufikia lengo letu,” alisema Mwidau.

Alisema kutokana na hali hiyo kila mara amekuwa akishiriki katika kuhamasisha maendeleo katika maeneo yote ya mkoa huo bila kujali uongozi wa kaa upo chini ya chama cha CUF au CCM.

“Tanga tuna ardhi nzuri na tuna kila sababu ya kujivunia jambo hili ingawa kukosekana kwa usimamizi madhubuti kwetu imekuwa ni kilio kikubwa kwa wananchi wetu tunaowaongoza, wabunge wote wa mkoa huu tuna wajibu wa kuliangalia hili,” alisema Mbunge Mwidau.

Katika ziara hiyo akiwa wilayani Pangani Mwidau, alisema kuwa amefurahishwa kuona wananchi na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwera kuamua kuchimba kisima kikubwa zaidi ya kilichopo sasa na katika hilo amefurahishwa kuona mchango wa awali wa mashine aliyoitoa imewezesha kujengwa kwa kisima kisima kingine kikubwa cha futi 45 na kipenyo cha nchi sita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. KAMA AKILI ZA WATANZANIA WOTE ZINGEKUWA KAMA HIZI TUNGEFIKA MBALI; MASLAHI YA TAIFA MBELE; HAKI KWA KILA RAIA MBELE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...