Picha na Habari-Mdau Abdulaziz Video,Lindi
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeandaa huduma za madaktari bingwa
kutoka hospitali ya Rufaa MUHIMBILI watakaotoa huduma katika
hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi (SOKOINE) kuanzia tarehe 8.4.2013
hadi tarehe 13.4.2013.
Uzinduzi wa huduma hiZi utafanywa rasmi siku ya jumatatu(KESHO) tarehe
8.4.2013,Mgeni rasmi ni mkuu wa mkoa wa Lindi pia uzinduzi huo
utahudhuriwa na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Ndg
Emmanuel Humba.
Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari,Meneja wa ofisi ya Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya Lindi,Bi Fortunata Kullaya alieleza kuwa
hatua hiyo imekuja ili kusaidia huduma kwa wateja wa Mfuko huo na
wagonjwa wengine ambapo wagonjwa wasio wateja wa Mfuko watatumia
taratibu za kawaida zilizopo katika kupata matibabu.
Hivi karibuni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Kwa kushirikia na Taasisi
ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)imetoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali
vya wajasiliamali katika wilaya za Lindi na Kilwa ili wajiunge na
mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) NA Kutoa msaada wa Mashuka kwa Hospital za
Wilaya ya Ruangwa na Kilwa
Meneja wa Ofisi ya Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya-Lindi,Bi Fortunata Kullaya akitoa taarifa ya ujio wa Madaktari Bingwa wanaoletwa na Mfuko huo na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kesho katika hospital ya Sokoine Lindi
Viongozi wa mfuko wa NHIF pamoja na WAMA wakiwa wameketi pamoja chini na waliohudhuria katika Elimu elekezi kwa vikundi vya wajasiriamali kujiunga na CHF Iliyofanyika katika kijiji cha Namangale-Lindi Vijijini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...