Juu na chini anaonekana Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Ikulu jijini Dar es salaam leo ambapo amekuwa na mazungumzo nao ikiwa ni mojawapo ya jitihada za Rais
Kikwete kutafuta muafaka na kutafuta utatuzi wa hali ya sintofahamu ambayo
inanyemelea nchi yetu katika kipindi hiki.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Ikulu jijini Dar es salaam leo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano) Mhe Steven Wassira.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Ikulu jijini Dar es salaam leo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano) Mhe Steven Wassira.
----
Viongozi wa dini wamewataka waumini
kote nchini kulinda amani na umoja uliopo
ili nchi isije ikaingia kwenye
mgawanyiko wa kidini na kuleta machafuko hapa Tanzania.
Wito huo umetolewa na viongozi wa dini
leo Ikulu ya Dar-Es-Salaam mara baada ya kikao cha pamoja baina ya viongozi wa
dini na Rais Jakaya Kikwete.
Viongozi hao wa dini wamefika leo
wakiongozwa na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza
la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Viongozi wengine wametokea Baraza la Kikristo
Tanzania (CCT) Seventh Day Advertist (SDA) na Baraza la Pentekoste Tanzania (PCT).
Mkutano huo umeanza kwa Askofu
Ngalalekumtwa kusoma tamko lao la pamoja kwa Rais Kikwete ambalo ndilo limetoa
muongozo wa mazungumzo hayo ya leo ambayo yamehusu Amani na Usalama wa Taifa na
migogoro ya kidini ndani ya jamii.
Mkutano wa viongozi wa dini ya
Kikristo Tanzania ni mojawapo ya jitihada za Rais Kikwete kutafuta muafaka na
kutafuta utatuzi wa hali ya sintofahamu ambayo inanyemelea nchi yetu katika
kipindi hiki.
“Nataka tuzungumze ni namna gani
tunaweza kutoka kwenye hali hii na tunakwendaje mbele zaidi na kuhakikisha nchi
yetu bado inakua ya amani na umoja kama
ilivyozoeleka”
Rais amesema na kutoa nafasi kwa viongozi wa dini kutoa maoni yao.
Viongozi hao wa dini wamemueleza Rais
Kikwete kuwa wanaunga mkono jitihada zake za kutafuta amani na kwa pamoja
wamekubaliana uandaliwe mkutano wa pamoja baina ya viongozi wa dini zote ambapo
masuala ya amani na umoja wa nchi utajadiliwa kwa kirefu.
Katika kikao cha leo pande zote
zimekubaliana kuwa kuna changamoto zilizoko sasa zinahitaji kutatuliwa haraka
iwezekanavyo ili kuepusha nchi kutumbukia katika mgogoro mkubwa zaidi, na pia
kukubaliana kuwa pande zote, kwa maana ya serikali na taasisi za dini,
zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha amani inadumu.
Kabla ya kikao cha leo , Rais amewahi
kukutana na viongozi wa dini ya kiislamu na kikristo mmoja mmoja ambapo alikua
akitafuta maoni na ushauri wa pande zote kabla ya pande zote hazijakaa pamoja
na kuwa na msimamo wa pamoja.
Kikao cha leo kimehitimisha jitihada
hizo na kinachofuata ni mkutano mmoja ambapo Rais Kikwete atakutana na viongozi
wa dini zote kwa pamoja hivi karibuni.
………...”MWISHO”……..
Imetolewa na:
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM
23
Aprili, 2013
Baba askofu Kitula wakilisha AIC baba
ReplyDeleteamani ndiyo lulu pekee inayng'aa idumishwapo. Nchi ya tanzania inabahati kubwa kuliko nchi nyingine ulimwenguni kote hivyo lazima tujivunie kwa zawadi hiyo pekee tuliyoruzukiwa na muumba. Unaweza ukapoteza simu na ukanua nyingine kariakoo au laini ukairenew namba ile lakini katika vitu ambavyo ni Ghali kuvipata ukivipoteza, ni AMANI. Sitaki turudi nyuma tuanze kunyoosheana vidole huyu kafanya hili na huyu lile maana tutakosa kuelewana na tukikosa kuelewana huenda tukakosa AMANI. Chakufanya ni kwamba tufanye tunavyofanya tuhakikishe Amani tuliyonayo inadumu na sikupotea hata kwa bahati au kwa kujisahau. Mwenzemungu tunakuomba uibariki tanzania na watu wake bila ya kujali Madhehebu na dini za watu wake. Aaamiyn!
ReplyDeleteAmani haipatikani kwa kutumiliwa viongozi wa dini pekee. Ni haki na wajibu kwa serikali kuu na za mitaa kushajihisha amani kwa vitendo kwa kuwatendea haki watu wote kwa usawa na uadilifu.Bila kusahau uwajibikaji kwa kila jamii na taasisi mbalimbali.
ReplyDeleteVyama pia vinanafasi kubwa sana kusimamia amani kwani ndio vyenye muamsho wa kasi sana kulinganisha na dini.
kwamtazamo huu sinashaka amani itadumu.
Kwa hy ma shekhe na ma ustadhi wao hawana maana? au mabubu? Jifikilie nyie.mxiuuuuuuuu viongozi wa ndo mnaoleta udini.Mungu awalaani wale wote wanaopiga vita waislam na uislam.
ReplyDelete