Uncle naomba unipe nafasi niweze kutoa ufahamu kuhusu Kabila la kizalamo na mji mkuu Dar-es-salaam na kariakoo kumekuwa na watu hapa nyumbani wasiojua maana ya hizi kwani hakuna somo mashule linalofundisha maana hasa.
Tukianza na kabila la wazaramu hawa ni watu walioweza kusafiri kutoka morogoro kwa mguu mpaka Dar wakati wakiwa wanatafuta dawa ya magonjwa aliyokuwa yanawasumbua kule morogoro hiyo ilikuwa mwanzoni wa karne ya 18 katika kusafiri huko kutoka morogoro mpaka Dar watu wengi sana walifariki njiani na kubakisha kundi dogo la watu waliokuwa na nguvu ndio walioweza kufika Dar.
kitendo cha kusafiri kutoka sehemu moja mpaka nyingine kilugha kinaitwa zaramo na ndipo watu hao wakaitwa wazaramo kwa hivyo wazaramo na warugulu ni ndugu kabisa ndo maana wanaitana wajomba(uncles) 
Baada ya kufika Dar wazaramo walifanikiwa kupata madawa mengi sana kutoka katika miti iliyokuwa karibu na bahari ya hindi dawa hizo zilikuwa za mizizi ya miti hiyo ilikuwa baharini na ndo hapo wazaramo wakaita hiyo sehemu wanayopata dawa za mizizi MZIZIMA.
 DAR-ES-SALAAM ni jina la kiarabu likiwa na maana ya sehemu salama ya kujihifadhi na sio bandari salama kama watu wengi wanavyojua. Na hii inatoka na vita kati ya wareno na waarabu kugombea sehemu ya msumbiji na baada ya waarabu kupata kichapo wakaja katika pwani ya Dar-es -salaaam kuja kujiifadhi KARIAKOO-jina hili ni la kingereza likiwa na maana ya sehemu ya kuchukulia wanajeshi wa kivita wakati wa vita ya dunia (CARRIER COPS) 
WAKWERE: hawa ni wazaramo walisukumwa kidogo nje ya Dar kuelekea morogoro Chalinze baada ya lile deal la kubadilisha dini kwa ajili ya kupata elimu kutoka kwa mzungu na kurudi katika dini yako kuaribika na wao wakabaki huko huko.
Cha msingi hawa wanaongea lugha moja na tamaduni zao ni moja Wazaramo, Warugulu na Wakwere. Naomba kama kuna mdau yoyote anayejua zaidi Maana ya majina ya makabila historia zao na hata maana ya majina ya mikoa kwani ni vizuri kujua nchi yako
Mdau United kingdom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Jifunzeni historia! Jifunzeni historia!

    Na Kiingereza pia: Carrier Corps!

    ReplyDelete
  2. Mie navyojua Wazaramo wa Dar-es-salaam walikuwepo toka zamani kuhusu Wazaramo wa Kiluguru nilivyosikia Zamani sana enzi za Mwanarumango kuna Bishara na kuna Mafuta kulikuwa na Mjerumani,Muhindi na Mwarabu pia Waarabu waliweza Kuowa Wazaramo sehemu zile Enzi za Biashara kwa Tabia za Wazaramo walikuwa wao wakipenda Kutahiri watoto wa kiume na hawakuruhusu kuchonga Meno na Kisa chwa Wazaramo ambao walikuwa Waluguru ni kwamba zamani sana Uzaramoni wakiona Mtu ni Mchawi wanamchoma Moto mbele za Watu ss Baazi za Familia zikaona zinaonewa wakaondoka na kuhama na kuhamia Morogoro ambapo ukitokea Mwanarumango sio mbali ila sasa kuhusu kutoka Morogoro kuja Dar-es-salaam hiyo ndio naisikia mie naongelea Wazaramo wa Kisarawe pande za Mwanarumango ndio walikuwa wakisema hayo kwamba walikimbia wengi sababu baazi ya Familia kuchomwa moto kwa kuambiwa walikuwa Wachawi na wenzao, na pia jua kuna na Wazaramo Bagamoyo pia. Wengi Dar-es-salaam walikuwepo na wengi waliolewa na Wazee wa Kiarabu. Maeneo yao yalikuwa sana Buguruni,Ilala enzi za Sultan anaijenga Mzizima na Wamanyema walikuwa maeneo hayo baadae miaka ya 80's ndio Wachaga wakaanza kuingia kwa wingi na kuijenga Mikocheni.

    ReplyDelete
  3. mimi siamini kitu mpaka nisome toka kwa anthropologists au local historian kama Mohammed Said aka SYDNEY

    hawa wengine naona wanaunganisha unganisha tuu

    ReplyDelete
  4. Dar-es-Salaam kweli ni Kiarabu ikimaanisha "Bandar(i) Salaam" yaani bandari salama na ilikuwa wakati wa dhoruba kali Bahari ya Hindi mabaharia wengi walitia nanga hapo. Mabaharia wa Kiingereza walipaita "Haven of Peace" meaning a harbor or port, or, any place of shelter and safety.

    BTW, zipo Darusalaam zingine ambazo ukiangalia zina the same meaning - I think one is in Yemen and the other in Brunei.

    ReplyDelete
  5. Jifunzeni Kiswahili! Jifunzeni Kiswahili!

    ... baazi... = baadhi
    ... Zamani sana enzi za Mwanarumango kuna ... Zamani sana enzi za Mwanarumango kulikuwa na
    ... Bishara ... = biashara
    ... Kuowa Wazaramo ... Kuoa Wazaramo

    (CHEKENI)!

    ReplyDelete
  6. WOTE HAMJUI KAWAIDA WAZARAMU MAANA YAKE WALIKUWA WATUMWA WA KUWANYENYEKEA HAO WAARABU MATOKEO WENGI WAKAWA MASHOGA BAADA YA KUONA KILA KIGINGI CHA MUARABU KILIKUWA KIMETAILIWA BASI NA WAO WAKAONA NI VIZURI WATOTO WAO WA KIUME KUTAILIWA VILE VILE , LAKINI BAADA YA MUDA WAKAJA WAJANA TOKA KIGOMA AMBAO WALIMGOMEA MUARABU KUWA WATUMWA , BASI HAPO WALICHUKULIWA WAZARAMU KADHAA WAKAPELEKWA HUKO MA UARABUNI KUWA MASHOGA NA KUWAHIDHI WAARABU BAADA YA KAZI NGUMU NDIO MAANA MMANYEMA AKACHUKUA KARIAKOO MPAKA LEO

    ReplyDelete
  7. Nakubali kabisa kuwa makabira haya yana uhusiano na msingi wao ni moja,kama vile walivyo wandereko au warufiji, wakichi,wanyagatwa,wanyangalio,wangindo ukiyaangalia kihistoria mama ni Matunmbi,makabila haya madogo na makubwa aliyo mkoa wa Pwani na Dar-es-salaam,yana udugu wa damu na utani wa jadi,pia wa asili ya ukarimu wa kupokea wageni na wageni nao wakajiona wapo "Salama" ndani ya Dar es salaam.
    Kinachisikitisha kwa sasa ni mpango na mikakati ya agenda za SIRI ya kuyahamisha makabila haya katika mkoa wa Dar es salaam, kwa visingizo mbali mbali za kimaendeleo,
    (B) Mbinu chafu na agenda za siri za kuifuta na kuizika kabisa historia ya Wazaramo na jiji la Dar es salam,kwa kubadili majina ya mitaa na vitongoji vya jiji.
    Mfano tumeona juzi bara bara ya Old bagamoyo road ikapewa jina lisilo na maana kwa watanzania "Mwai Kibaki" !
    Na kila kiongozi anataka kujenga kumbu kumbu kwa kuipa jina bara bara au mtaa fulani.
    Mtaa wa kichwele amabo sasa ni uhuru st,ulikua na maana kwa sababu mtaa wa uhuru ndiko alipopita mwalimu Nyerere akitokea uwanja wa ndege akirudi kutoka UN na wazaramo wakamwimbia "Baba Kabwela UNO"
    Hawa wazaramo walioimba leo wanafukuzwa jijini kiujanja ujanja,

    ReplyDelete
  8. nyie nyote hamjui story kamili ya wazaram..maana halisi ya uzaram ni mzaliwa humu, yaani mzawa maana halisi ni mzawa wa pwani upande kutoka morogoro mpaka ukanda wa rufiji asili ya wazaram kwanza ni watu wengi wametokana na makabila ya uhamiaji ambayo wachaga wagogogo wanyamwezi ambao walikuwa katika kuja kutafuta maisha au kikazi pwani na wengine ni ilikuwa biashara ambayo walikwama katika mashamba yaliyo kuwa upande wa pwani ya kilwa na bagamoyo sasa wengi walibakia na wamezaliwa pwani kwahiyo ni wazaramumo..lol

    ReplyDelete
  9. Good on you! Thanks for the very informative article, am very impressive with the origin of Kariakoo, I really didn't know about zat. Thanks very much mdau.

    ReplyDelete
  10. weeeee muongo sana.swali wazaramo walipotembea kwa mguu mpaka dar walipofika dar waliwakuta watu gani hapo dar? na waarabu hawajapigana na wareno ile msumbiji ni nchi ya waislam na jina limetokana na mzee mwenyewe sheikh musa bin mbeki. wazungu hawajui kutamka musa bin mbeki wakawa wanatamka mozambique. usiwaongopee watu hapa.

    ReplyDelete
  11. stori za kijiwe tuu hizi,kila mtu ana yake.

    ReplyDelete
  12. Hata Wasukuma na Wanyamwezi ni hivyo hivyo. Wote walikuwa wanyamwezi. Ila baadhi yao hawakupenda baadhi ya watemi wa kinyamwezi hivyo wakaamua kuhama na kuelekea kaskazini ya temi za kinyamwezi. Walipoama wakawa wanajitambulisha kama watu wa kaskazini yaani wasukuma. Neno wasukuma maana yake ni "people from the north" kwa maana ya wanyamwezi waliohama kwenda kaskazini wakawa wakijitambulisha hivyo. Hivyo wakawa wasukuma lakini kimsingi ni watu wamoja na lugha moja. Ila kutokana na kuhama hata lugha zikapata maneno machache yakawa tofauti kama ilivyo kwa kiingereza cha uingereza na kile cha Marekani. Lakini wote wanazungumza lugha moja kama ilivyo kwa wasukuma.

    ReplyDelete
  13. HIZI STORY ZA KUUNGAUNGA WALA HAZIMAKE SENSE!

    ReplyDelete
  14. Hakuna cha kuchekesha hapo, amejitahidi kuelezea anachofahamu. Mbona wewe huja elezea chochote. Usipende kunyosha kidole kwa mwingine kumbuka vinne vinakuangalia wewe.
    11:37

    ReplyDelete
  15. JAmani wewe historia ya wazaro kweli umeivuruga, ngoja nikwambie mie nimesoma kitabu kinaitwa "DESTURI ZA WASUHELI" kiliandikwa na mjerumani ambae alistudy sana pwani kuanzia pangani mpaka mbwamaji na kati kati, sikiliza historia ya wazaramo.

    Enzi hizo katika karne ya 18 kulitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe huku mzizima ambapo wakati huo kulikuwa na mkubwa wa maeneno hayo, akamuomba mtemi wa wanyamwenzi amuazime wanajeshi wake, wale wakasafiri mpaka wakafika dar es salaam, kufika hapa wakapigana mpaka! vita ikamalizika, wale wakawa hawajaridui, yule mtemi wa wanyamwenzi akawatuma askari wake wengine waje kuuliza mbona hawarudi na wanasikia hali ni shwari sasa, wale wanyamwenzi walipofika huku kwa wenzao wakasema sisi haturudi "TUMEZARAMA" ndio ikaanza hiyo historia ya wazaramo maana wahamiaji na hii si wanyamwenzi peke yake kama unavosema inawezekana na waruguru nao walikuwa wanarudi kwao kama histor ya mdau hapo juu na mkubwa wa wazaramo baadae akawa PAZI KILAMA, amezikwa pale BAgamoyo kwa Mwana makuka, nenda kuna shule pale na kaburi lake na la mkewe lipo pale, alikuwa balaa huyo pazi kilama.

    Historia ya KAriakoo nayo umeipindisha, eneo la soko la kuu pale KAriakoo kulikuwa ndio eneo ambalo wanajeshi kwa jina la "carrier corps" yalikuwa ndio makazi yao ya mazoezi na vinginevo ndio watu tena karia koo mpaka leo lo; mie mzaramo pure na nimeisoma historia yangu, inawezakamna kabisa ikawa mchanganyiko wa makabila mengi WALIOZARAMA, lakini wengi ni wanyamwenzi na waruguru kama unavosema na ukienda unguja wengi wao ni wanyamwenzi leo wanajifanya washirazi hebu mchukuwa mzanzibari mmoja umuulize kabila lake atakwambia mshirazi lakini root yake ni mnyamwenzi.

    ReplyDelete
  16. Hii ndio shida ya wabongo,jamaa kaeleza kutokana na uelewa wake,mwisho kaomba kama kuna anejua zaidi nae atoe maoni,tueleweshane taratibu na vizuri,sio kutupiana maneno ya kashfa na upuuzi.

    ReplyDelete
  17. Huyo anayesema wazaramo walikuwa mashoga hiyo hadithi umeitoa wapi? Kama kitu hujui uliza au fanya utafiti tu mwenyewe usiwe unakuja na maneno ya kihuni, ushoga ni mtindo wa wazungu na hapa Tanzania watu wanaoishi kwenye miji na kufanya biashara na ndio ambao wenye nchi yao toka enzi za Adam ni waislam kwa hiyo suala la kutahiriwa ni wajibu wa imani yao ya dini halihusu ushoga. Ushoga umeletwa na wamisionari ambao ulaya na america wamewafunga kibao na ndio maana imani ya dini ya kikristo kwa wazungu imekwisha na sasa wanaruhusu ushoga katika nchi zao sababu imani ya dini waliyokuwa nayo hawaielewi na hawaikubali. Mwandishi ameleta mwangaza kidogo kuhusu uhusiano wa haya makabila ( Wazaramo, wakwere na waluguru) na amefungua debate ambayo matokeo yake wengi tutaelimika wacha kuleta maneno yasiyokuwa na maana.

    ReplyDelete
  18. Twila mtumbiApril 24, 2013

    Haya mmejitahidi sana kutoa maoni mazuri lakini bado. Alafu tujaribu kusoma tulichokiandika kabla kukituma itakuwa vizuri sana, sababu tunachapia sana lugha du. Kingine tujaribu kuelimishana sio kubishana na kashfa sio vyema.mimi pia kizaramo halisi najua kiasi napenda kujua zaidi lakini kashfa sio vyema.

    ReplyDelete
  19. Hmmmmmmmm Nimeipenda hii KARIAKOO kumbe ndio hali halisi Asante sana mdau kwa kututoa mchanga wa macho sisi wengine,wataalamu wa historia msaada kwenye tuta tafadhali kama inawezekana : WAHAYA NA WAUGANDA WANAINGILIANA LUGHA ZAO JE HAPO WANA UHUSIANO WOWOTE ? Msaada tafadhawali

    ReplyDelete
  20. Ndugu zangu wapendwa. Kwa mwenye nia safi ya kujua asili ya Wazaramo na Dar es Salaam na mkoa wa pwani mzima, waulizeni Katundu na Pazi ndio waliokuwa Chief na wamiliki wa mikoa ya pwani ndio mtapata ukweli. Bila ya hivyo tutapotezana. Shukran.

    ReplyDelete
  21. Tuulizeni tuwapeni true history of Zaramo tribe. Kiumeni kwa babangu ni Nyakatundu na kikeni kwa babangu ni Nyapazi.

    ReplyDelete
  22. Suala la Mzizima eti dawa ya mizizi si kweli. Ninavyofahamu Mzizima inatokana na neno zizimi yani utulivu. Kama mahala pana utulivu hakuna zogo panaitwa Mzizima. Na ndiyo maana Waarabu wakaita mji wa Mzizima Dar es Salaam yani Mji wa Amani. Kwenye hiyo historia kuna mambo mengi hayapo sawa. Kama kusema wazaramo ni wahamiaji si kweli. Au kusema kuna koo mbalimbali zilitoka bara ndiyo zikaunda kabila la wazaramo. Wandengereko, Wangindo na Wamatumbi ni miongoni mwa makabila ya kusini huko Lindi na Mtwara na yamekuja Uzaramoni kitambo mbona hayaitwi Wazaramo? Au ndiyo nyinyi mnaodhania Wandengereko Wamatumbi na Wangindo nao ni Wazaramo? Eleweni kuwa kuna sababu iliyosababisha Wazaramo kuitwa jina hilo. Na hata Waluguru kuitwa hivyo kuna sababu pia. Tena sababu zenyewe zinatokana na kilimo, biashara na miamala ya kisiasa kwa wakati huo kati yao na wageni mbalimbali kutoka Bara Hindi na Bara Arabu. Nikipata wasaa nitachambua sababu hizo moja baada ya nyingine inshallah.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...