Lady Jaydee
Katika mwaka huu wa 2013, inatimia miaka13 tangu nianze  kazi ya muziki.
Nashukuru MUNGU tuko pamoja na pia nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea kusupport muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii.
Nashukuru vyombo vyote vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya muziki Tanzania bila kujali maslahi binafsi.
Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE katika muziki.
Na mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV.
Sherehe ya miaka 13 ya Lady JayDee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la 'NOTHING BUT THE TRUTH' ambayo ina jumla ya nyimbo 10.
Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za JayDee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.
Nawakaribisha wote tufurahi pamoja
Na Mungu Awabariki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana Lady Jaydee.Wewe ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wa TZ.Sherehe zinafanyika wapi hiyo siku,Ukumbi,Uwanja,n.k??

    David V

    ReplyDelete
  2. Hongera sana dada, tupo pamoja. Tutakupa support ya nguvu. Nakupendaga sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...