Lady Jaydee
Katika mwaka
huu wa 2013, inatimia miaka13 tangu nianze
kazi ya muziki.
Nashukuru
MUNGU tuko pamoja na pia nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea kusupport
muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii.
Nashukuru vyombo
vyote vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya muziki Tanzania
bila kujali maslahi binafsi.
Tumeandaa sherehe
kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE katika muziki.
Na mdhamini mkuu
kwa upande wa media ni East Africa TV.
Sherehe ya miaka
13 ya Lady JayDee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda
kwa jina la 'NOTHING BUT THE TRUTH' ambayo ina jumla ya nyimbo 10.
Katika sherehe
hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za JayDee nikishirikiana na baadhi
ya wasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika
Ijumaa tarehe 31 May 2013.
Nawakaribisha
wote tufurahi pamoja
Na Mungu Awabariki
Hongera sana Lady Jaydee.Wewe ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wa TZ.Sherehe zinafanyika wapi hiyo siku,Ukumbi,Uwanja,n.k??
ReplyDeleteDavid V
Hongera sana dada, tupo pamoja. Tutakupa support ya nguvu. Nakupendaga sana
ReplyDelete