Waziri mkuu mstaafu, Mh. Frederick Sumaye akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya sita ya wahitimu 1029 wa chuo cha ualimu mjini Singida. Kulia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi na kushoto ni mmiliki wa chuo cha ualimu Singida, Martin Makuza.
Mkurugenzi mtendaji wa Prime Education Network (PEN) Tanzaia, Martini Mkauza akitoa nasaha zake kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha ualimu cha Singida mjini. Kulia ni waziri mkuu mstaafu,Frederick Sumaye.
Waziri mkuu mstaafu, Mh.Frederick Sumaye akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu 1,029 wa chuo cha ualimu Singida.
Baadhi ya wahitimu wa chuo cha ualimu Singida,wakifuatilia kwa makini hotuba ya waziri mkuu mstaafu Mh. Frederick Sumaye (hayupo kwenye picha) wakati akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo hicho.
Kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Manguanjuki manispaa ya Singida kikitoa burudani kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha ualimu mjini Singida.
Mmoja wa waandishi wa habari,Damiano Mkumbo akiwajibika kupata picha safi kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha ualimu mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mwalimu QUEEN MLOZI (Mama Mlozi). Kweli unastahili wadhifa huo na ikiwezekana zaidi ya hapo. Nakumbuka juhudi zako na malezi yako kwa jumla, wakati huo ukiwa mkufunzi katika chuo cha ualimu Kigurunyembe. Sitokusahau katika somo lako la UONGOZI. haikuwa kinadharia tu, bali hata kiutendaji, you deserve it and no doubt you can do it MORE!

    Nakuombea kila la kheri, MOLA akulinde na kukuongoza vyema, pia ufanikiwe zaidi na zaidi ya hapo ulipo. INSHA ALLAH.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...