Pamoja na Mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam, jana na uwanja wa Netoboli na wa Mpira wa miguu TCC kujaa maji lakini bado timu za TASWA FC na Netiboli ya TASWA Queens, ziliibuka na ushindi mnono katika Bonanza la Pasaka dhidi ya timu ya Kiliflora ya Arusha. Hapa wachezaji na viongozi wa timu hizo wakijitahidi kuondoa maji katika uwanja wa Netiboli kabla ya kuanza kwa mtanange huo, ambao ulimalizika kwa TASWA Queens kuibuka na ushindi wa mabao 28 -8. Picha zote na Nasma Mafoto
Majuto Omari wa Taswa Fc (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Kiliflora ya Arusha, ambapo hadi mwisho Taswa Fc Iliibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Iman wa Taswa Queens, akitupia moja kati ya magoli 28 waliyofunga.
Mtanange unaendelea.....
Beki wa TASWA Fc Muhidin Sufiani (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa Kiliflora ya Arusha.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Huyo mwenye jezi number kumi anahitaji mazoezi ya ziada mhhhh!
ReplyDelete