Pichani kushoto ni aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye usiku wa kumbu kumbu ya Marehemu Steven Kanumba,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh Yusuph Mwenda akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba,kwa niaba ya Mh Rais Jakaya Kikwete,kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufarikii kwa nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko.Kumbukumbu hizo zimefanyika jana jioni kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wa tasnia hiyo,wasanii wa muziki na kada nyinginezo mbalimbali,aidha katika Kumbukumbu hiyo pia kulizinduliwa Filamu ya mwisho aliyokuwa akiigiza Marehemu Kanumba kabla ya kufariki iliyoitwa Love & Power.
Pichani kushoto
ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akipokea tuzo
ya heshima kutoka kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba,kwenye maadhimisho
kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufarikii kwa nyota huyo wa Filamu
hapa nchini na kwingineko,Steven Kanumba.Kumbukumbu hizo zimefanyika jana jioni
kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na wasanii
mbalimbali wa tasnia hiyo,wasanii wa muziki na kada nyinginezo mbalimbali,aidha
katika Kumbukumbu hiyo pia kulizinduliwa Filamu ya mwisho aliyokuwa akiigiza
Marehemu Kanimba kabla ya kufariki iliyoitwa Love & Power.

Mwakilishi kutoka
Kampuni ya Clouds Media Group,Zamaradi Mketema akipokea tuzo ya heshima kwa
niaba ya kampuni hiyo iliyotoa mchango mkubwa katika tasnia ya Filamu hapa
nchini,kutoka kwa Mama yake,Marehemu Steven Kanumba,kwenye maadhimisho ya kumbu
kumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu afarikii nyota huyo wa Filamu hapa nchini
na kwingineko,Steven Kanumba.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama yake Marehemu Kanumba,kwa mchango wao mkubwa walioutoa kwenye tasnia ya Filamu hapa nchini.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...