Mnamo tarehe 23 April, 2013 majira ya saa tisa alasiri, huko wilayani Liwale mkoani Lindi, kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni wakulima wa Korosho walijaribu kuzuia gari lililokuwa na malipo ya korosho wakipinga malipo ya pili ya Korosho na kuanza kufanya vurugu na uhalibifu mkubwa wa mali, ambapo mpaka sasa taarifa za awali zinaonyesha kuwa nyumba kumi na nne (14) zimechomwa moto, baadhi ya mifugo imejeruhiwa na kuangamizwa na kufanyika uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema ametuma timu maalum ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCP Issaya Mngulu kwenda kuongeza nguvu mkoani humo kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa katika kuhakikisha kuwa hali ya amani na utulivu inarejea haraka na wale wote waliohusika kufanya vitendo vya uhalifu wanakamatwa na kufikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake, mpaka sasa jumla ya watuhumiwa kumi na tisa (19) wamekamatwa kwa mahojiano.
Aidha, Jeshi la Polisi nchini linalaani vikali vitendo hivyo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi na badala yake kuwataka wananchi kufuata njia ya kufanya majadiliano pale ambapo kutakuwa na migogoro ya aina yoyote ndani ya jamii. Majadiliano yatasaidia kuepusha madhara yanayojitokeza ikiwemo watu kupoteza maisha, uhalibifu wa mali na misongamano ya wahalifu magerezani.
Wakati hatua hizo za kisheria zinaendelea kuchukuliwa, Jeshi la Polisi linawaomba wananchi kuwa watulivu na waendelee kutoa ushirikiano ili kuweza kuwabaini wahalifu hao wachache wanaochochea vitendo vya vurugu na kufanya uhalibifu wa mali ili hatiamae waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Taarifa zaidi juu ya tukio hili zitaendelea kutolewa na uongozi wa mkoa wa Lindi baada ya tathmini ya uharibifu uliofanyika kukamilika.
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (TZ).

Tatizo liko kwenye kutenda uadilifu. Kabla ya stakabadhi ghalani hatujawahi kuona fujo kama hizi. Na kwa kawaida kipindi hicho wananchi walikuwa wanapeleka korosho zao gulioni; wanauza na kupewa hela siku hiyo hiyo. Yani korosho zinapimwa kulingana na kiasi cha hela kilichopo. Hii ilikuwa ni njia bora; kwani mtu anapata chake siku hiyo hiyo. Na kipindi cha msimu wa korosho sura za Watanzania zilizokuwa zinategemea zao hilo zilikuwa zinameremeta. Lakini siku hizi ni kinyume chake. Watu wamekata tamaa kabisa na hali zao ni mbaya sana.
ReplyDeleteHalafu naona kweli haki hakuna hapa. Ni rahisi kumkopa mkulima Mtanzania lakini ni vigumu sana mkulima Mtanzania kupata mkopo. Ndiyo maana kuna msemo kwamba haki thamani yake ni "infinity" au "undefined". Kwa maana nyingine haki itafutwe kwa gharama yeyote ile.
Sasa hapo ukiangalia unasema kuwe na majadiliano ni sawa; lakini kinachotakiwa kufanyika kinajulikana. Mkulima anataka apewe hela yake kutokana na jasho alilolitoa shambani kwa taabu sana. Usiku kucha wanatembea mashambani kupulizia mikorosho. Kidogo alichopata ananyang'anywa mchana kweupee; huu ni wizi wa kutumia makaratasi na nafikiri waliohusika wote waache kazi na washitakiwe kwa matumizi mabaya ya madaraka.
Wanaotuongoza wamwogope yule Aliyewaumba. Vinginevyo hisabu ni ngumu siku ya hisabu.
Na kwa njia rahisi mfumo uliopo (stakabadhi ghalani) wa ununuzi haufai kisayansi.Sayansi na uadilifu haviwezi kupingana hata siku moja; ni kitu kimoja.
Na kuanzia msimu ujao serikali iweke kima cha chini cha kununua korosho kwa kuangalia gharama za Mkulima anazotumia kuzalisha korosho. Yani kufanyike SCIENTIFIC ANALYSIS ya kutafuta kima cha chini cha korosho; siyo kukaa tu ofisini na kusema kima cha chini cha korosho ni shilingi 1000 kwa kilo. Halafu anayetaka kununua korosho aende moja kwa moja kwa wakulima anunue na kuwapa hela yao siku hiyo hiyo; bila kukopana.
Huko si kuwajibika; na kwa ukweli anayehusika anatakiwa aache kazi kwa kuwa ameshindwa kufanya kazi kama nchi yetu ilivyoamua kuanzisha buro ya kuangalia PERFORMANCE ya utendaji kazi kwa waliopewa wajibu wa kuwatumikia Watanzania.
Tuchape kazi Watanzania tulete mabadiliko ya kweli nchini mwetu ili haki itendeke kwa kila raia, na tuondoe mabaki ya ukoloni ili uhuru kamili upatikane; Muumba atupe nguvu kwa hilo na Ajaalie amani na upendo nchini mwetu.