Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah
Kigoda akisoma hotuba ya Wizara yake Bungeni
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na
Naibu wake Mh Gregory Teu wakisikiliza kwa makini michango ya Wabunge kwa
Wizara yao.
Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na
Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakifuatilia mawasilisho ya bajeti yao
Bungeni mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiwaongoza
Mawaziri na Naibu Mawaziri kuwapongeza Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt
Abdallah Kigoda na Naibu wake Mh Gregory Teu baada ya
Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah
Kigoda na Naibu wake Mh Gregory Teu wakipongezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Bi Joyce Mapunjo nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Bajeti ya Wizara hiyo
kupitishwa na Bunge.
Watumishi na Viongozi wa Wizara ya Viwanda na
Biashara wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya ukumbi wa Bunge baada ya Bajeti
yao kupita.


Muchuzi hawa wote waliovaa sare(vitenge) kuja dodoma kusikiliza just kupitishwa kwa budget ya wizara wanalipia gharama za kukaa dodoma na nani? Kodi ya wananchi inateketea kwa mambo ya hovyo.
ReplyDeleteAaaaaaa siku hizi sae imeingia bungeni?
ReplyDeleteWao! Nii ukoloni au utamaduni huu!
Hayiiiiiiiiiiiiii Afrika tutafika kweli, sare za wizara??????? Au office hii ina uniform? mboni kazi
ReplyDeletehii pesa ya kushonesha sare zote hii wametoa wapi hawa watumishi wa serikali?ni fungu maalum au pesa yao??
ReplyDeletena hv kweli kuna uhitaji wa kundi lote hili la watu kwenda kwenye kusoma tu budget?nani amebaki ofisini kuhudumia watu?nani amegharamia perdiem za hawa wote huko?
me nadhani ifike mahali hata kama hatuheshimu kubana matumizi tumuogope Mungu kwa maana kuna siku tutajibu mbele zake kwa madhila tunayowafanyia maskin wa tz
mdau
france
Ni wengi!
ReplyDeleteKundi lote hili? Huu ni ufujaji wa pesa za walipa kodi. Tuanze kuwa serious jamani hii aibuu
ReplyDeleteKWA NINI BAJETI IKIPITISHWA BUNGENI VIONGOZI WANAFANYA SHEREHE NA KUFURAHI SANA NA PIA KUPONGEZANA????
ReplyDeletemichuzi hawa jamaa inatakiwa watueleze hilo fungu wamelitoa wapi na je mambo ya msingi yamekamilika hadi kuamua kuzitumia hela zetu katika mambo ya kuwapeleka wadau dodoma
ReplyDeleteAh wakati mwingine mi naona wabongo tumezidi ushamba. Wizara kama ya Viwanda na biashara ina taaisi 20 na mashirika kibao chini yake. hata wakituma wawakilishi wawili kila taasisi ni rahisi kuona kuwa wapo wengi. Na vitenge vyenyewe mbona vya bei poa tu, kila mwaka huwa wanavaa na siku za kazi kuna siku moja kwa wiki huwa wanavaa hivyo.
ReplyDeleteMaoni mengine pumba kabisa, badala ya kufikiria kuona mchango wa Wizara kwa maendeleo ya nchi watu wenye mawazo finyu mnaona vitenge na kuhoji gharama. Nonsense kabisa. Hongera zenu Wizara ya Viwanda, sisi watu wa Singida tunasubiri viwanda vya kuongeza samani kwenye alizeti zetu tujae mahela
ReplyDeleteKama kuna Wizara imenifurahisha ni hii ya Viwanda na Biashara. Hawa watu wakipewa fedha za kutekeleza mipango yao ni wakombozi wa Taifa. Wingi bungeni sio hoja, vitenge cheap kama vile sio hoja, tena product za viwanda vyao, bora tuwapongeze kwa uzalendo. Ma Wizara ya ufisadi hamyajui nini? Ma trilioni yanapita nyie hamuoni? acheni ushamba
ReplyDeleteNyie mmnaoilaumu wizara ya viwanda kwa kutumia pesa vibaya kwa kununua sare muwe mnafanya utafiti kwanza kabla ya kukurupuka mimi nilichukua picha mojawapo nikaenda yenye sare ya kitenge nikauliza kwa watu wanaouza vitenge wakaniambia kitenge kimoja cha aina hiyo hakizidi TSh.10,000/=(elfu kumi ) tena kinaweza kuwa chini ya hapo kwa mfano wizara hiyo imeamua kuwanunulia watu 300 vitenge hivyo ukipiga kwa hiyo 10,000/- utapata Tsh.3,000,000/=(Milioni tatu tu) ukifuata uhalisia huo ni uharibifu wa fedha kweli? na kama watakuwa wamenunua vitenge pungufu ya hapo inamaana gharama ilikuwa ndogo zaidi ya hiyo niliyokadiria. kwa mtu anayejua kufanya mahesabu atakubaliana na mimi kuwa wizara hiyo ni moja ya wizara zinazotumia fedha vizuri kwani wangekuwa wanatumia vibaya wangenunua hiyo misuti yenye gharama kubwa badala yake wamethamini bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.
ReplyDeletemimi sina shida kabisa na wizara hiyo tena nawaasa muendelee hivyo hivyo ili na wengine waweze kuiga mfano wenu wathamini bidhaa zetu ili viwanda vyetu viendelee.
Michuzi hizi hoja za vijiweni na usiwe unazipa nafasi kwenye blog yako. Mimi nimesoma hotuba ya Dr Kigoda kikamilifu, ipo kwenye website yao, nimeona vitu kibao vya msingi. Nadhani hebu tuwapigie debe wapate fedha badala ya huu upuuzi wa wapo wangapi bungeni. Hata kama mnaowakosoa ni wapinzani wao, kuweni fair kwamba hawa watu wanafanya kazi tena katika mazingira magumu, tuwatie moyo na sio ukosoaji wa hoja za kipuuzi. Mbona vitenge vyenyewe vinaonekana chakavu?
ReplyDeleteDr.Kigoda mnamuonaje?
ReplyDeleteMnafikiri yeye atakuwa mfujaji wa Fedha za Umma wakati yeye ni Economist wa kuaminika?
Kuweni na Point za maana mnapo toa Maoni yenu, mbona Wizara za Kifisadi hamjazitolea mifano zile zinazonunua Masuti?
Kunya anye hadi Tembo, lakini akinya Bata kaharisha!
Fuatilieni Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara muone kazi!
ReplyDeleteAchaneni kabisa na Mhe. Dr.Kigoda ongeeni maneno yanye maana.
Nimefarijika kujua kuwa kuna watu wanasimamia kwenye ukweli na haki mimi nakubaliana moja kwa moja na wachangiaji wote wanaopenda haki na ukweli na sio wale wanaotumia hii mitandao kupotosha umma.
ReplyDeletekwa bahati nzuri nilifanikiwa kuhudhuria maonesho ya saba saba na nikatembelea banda la wizara hiyo ambapo nilikuta wawakilishi wachache wa wizara pamoja na wawakilishi wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo ambapo nilifurahishwa sana kuona wote wakiwa wamevaa sare moja tena vitenge nikataka kujua kwanini wanavaa sare za vitenge tena vya bei nafuu nikaelimishwa kuwa kauli mbiu yao inahamasisha watanzania kuthamini bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vyetu vya ndani ili kukuza uchumi wetu.mimi nafikiri tungetumia mitandao kama hii kusaidia wizara hiyo kuhamasisha watanzania wenzetu kutekeleza kauli mbiu hiyo na si vinginevyo.
Na kama hao waliondika kuwa wizara hiyo imepeleka watu wengi Bungeni hawajui ni taasisi ngapi ziko chini ya wizara hiyo mimi nawashauri wasikose kuhudhuria maonesho ya mwaka huu ili wajionee wenyewe hapo ndio watajua kuwa wizara hiyo pamoja na taasisi zake zilipeleka watu wachache na kwa jinsi walivyokuwa wawazi wakavaa sare je wewe unajua wizara nyingine zinapeleka watu wangapi? tena wanaweza kuwa wengi zaidi hawavai hata sare hivyo si rahisi kuwatambua. hivyo acheni chuki zenu zisizokuwa na msingi mfanye mambo ya maana yanayojenga.
Akili ndogo hujadili mambo mepesii na kuacha mambo ya maana. Wizara ya viwanda na biashara chapeni kazi, msikatishwe tamaa na hizi hoja za vibarazani. Maneno hata kwenye kanga yako. Njooni Mbinga tumalizane kwenye makaa ya mawe
ReplyDelete