Mwenyekiti wa  Taasisi ya Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (kulia) akisalimiana na mwendesha baiskeli wa masafa marefu, Alan Knight katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alan hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.   Wengine ni baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo.
  Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sikoseli Tanzania, Mhe. Abdallah Mwinyi (kuli) akisalimiana na mwendesha baiskeli wa masafa marefu, Alan Knight katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alan hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.   Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Grace Rubambey.

 Mwenyekiti wa Taasisi ya ugonjwa wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey  (kulia) akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia walikuwa wakimkaribisha mwendesha baiskeli Alan Knight (wa tatu kushoto), ambaye hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam 
 Mwambata wa Kisiasa kutoka Ubalozi wa Canada nchini, Dk. Carol McQueen  (kulia) akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia walikuwa wakimkaribisha mwendesha baiskeli Alan Knight (hayupo pichani), ambaye hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Ubalozi huo ulitoa shs milioni 30 kwa ajili kusaidia suala la utoaji elimu kwa jamii kuhusu sikoseli.
 Baadhi ya watu waliohudhuria hafla ya uchangishaji fedha kwa ajili ua ujenzi wa kituo cha kuhudumia wagonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa katika hafla hiyo ambayo jumla ya shs milioni 54 zilichangishwa. Ujenzi wa kituo utagharimu shs milioni 75.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2013

    Siku zijazo unaporipoti taarifa kama hii uandike sickle cell na si sikoseli.Tutafika tu ni kuelekezana kidogokidogo mpaka tutakaa sawa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2013

    Aliandika kwa Kiswahili so Kingereza Anym No. 1.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2013

    sikoseli ni neno la kiswahili; kwa hiyo yuko sahihi. Ni neno zuri tu katika sayansi ya viumbe kutumika kwenye viumbe. Ukizingatia kwamba kwenye tulikuwa hatuna neno hilo hapo awali. Lugha nyingi ndivo wanavyofanya kama teknolojia fulani imeibuliwa kwenye nchi nyingine inayotumia lugha tofauti. Kwa hiyo mwandishi uko sahihi na endeleza libeneke...

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2013

    We mtoa hoja wa kwanza umechemsha, sickle cell in Kizungu, Kiswahili cha sickle cell ni MUNDU KIINI.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2013

    Mh Kiswahili cha sickle cell ni sikoseli, nina mashaka na huo utafsiri! Kwa hiyo mtoa hoja wa kwanza yuko sahihi kabisa. Wataalamu wa afya hasa madaktari tusaidieni kwa hilo! Mundu kiini ukijaribu kugoogle! Ila sijui kama ndio linalotumika kwa kiswahili! Mh lugha hizi na ugumu wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...