Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema akimvisha cheo kipya cha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Thobias Andengenye ambaye hapo awali alikua Kamisha Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP). Hafla hiyo fupi imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wawili kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi na maofisa kumi na tisa kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi kuwa Naibu Kamishna wa Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema akimvisha cheo kipya cha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Alice Mapunda ambaye hapo awali alikua Kamisha Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP). Hafla hiyo fupi imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wawili kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi na maofisa kumi na tisa kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi kuwa Naibu Kamishna wa Polisi.
Kamishna mpya wa Jeshi la Polisi ambaye pia ni Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam,CP Suleiman Kova akionyesha ishara ya pongezi mara baada ya kupandishwa cheo cha Ukamishna wa Polisi,Kamanda Kova hapo awali alikua Naibu Kamisha wa Polisi (DCP). Hafla hiyo fupi imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2013

    YHongereni kwa kutunukiwa vyeo. Hii ni ishara ya kazi nzuri mnayoifanya. Jamani niambieni KamandaTossi yuko wapi?Ama alishaastaafu? Yule alikuwa jembe kwelikweli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2013

    Anony hapo juu nakubaliana na wewe kabisa.

    Kamanda Tossi alikuwa Jembe bwana.

    Naukumbuka ile operesheni aliyoendesha kule Msitu wa Biharamulo nadhani kuwaondoa wale Majambazi waliokuwa wakijificha msituni mule! We acha tu!

    Mpandisheni nae cheo bana!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2013

    KAMANDA TOSSI ALIKUWA JEMBE,UKIMUONA HUWEZI KUMDHANIA KWANI ALIKUWA MPOLE NA MNYENYEKEVU KWA WATU WA RIKA ZOTE,ISIPOKUWA UKIINGIA KWENYE ANGA ZAKE UTAJUTA.ILE OPRESHENI YA ULE MSITU ILIWAFYEKA MAJAMBAZI WENGI TOKA JIRANI ILA HAKUDUMU KULE BK.SASA HIVI AMESTAAFU NA YUKO TANAPA ANAPAMBANA NA MAJANGILI YA PEMBE ZA NDOVU.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2013

    Kamanda Tossi amekuwa mkufunzi wa jeshi la wanyama pori baada ya kustaafu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...