Tanzania imetengeneza historia mpya kwenye ngumi za kulipwa nchini Thailand baada ya mabondia wake kuwa wanapigwa kila mara wanapokwenda kuiwakilisha nchi na bara la Afrika. 
Safari hii JEMBE, kijana mtanashati anayeinukia kwenye masumbwi Jonas Segu kutoka katika ukumbi wa mazoezi wa Respect Gym Boxing Club ya Mabibo Loyola chini ya kocha Christopher Mzazi ameonyesha kipaji kikubwa cha kusukuma msumbwi alipoushangaza umati wa maelfu ya wananchi wa Thailand pamoja na nchi za ukanda wa Indo-China. 

 Segu alikuwa anachuana na bingwa wa IBF katika mara la Asia Pacific Patomsuk Pathompothong kutoka Thailand katika uzito wa Light Welter ambaye ni bondia namba 7 duniani katika viwango vya IBF. Mpambano wao ulifanyika katika jiji lenye mahekalu ya dhahabu la Bangkok na kurushwa na television katika nchi zote za ukanda wa Indo-China za Laos, Myanmar, Cambodia, Vietnam na Thailand yenyewe. 

Mpambamo wa Segu na Pathompothong ulianza kwa bondia wa kitanzania kuchomoka kama upinde kwenye kona yake na kumshambulia Pathompothong kwa makonde mazito ya kumshikisha adabu. Segu alitupa makonde ya mchanganyiko na kumzidi Pathompothong kutokana na uzito na umakini wa ngumi zake. Kwa kipindi chote cha raundi ya kwanza ilimbidi Pathompothong ajilinde na kukimbia akizunguka ndani ya ulingo ili kudhoofisha masumbwi ya Segu aliyekuwa anayachanganya kama mashine ya kukomboa mpunga ambao unalimwa kwa wingi nchini Thailand! 
Jonas Segu alikuwa chini ya uangalizi makini wa bondia maarufu mstaafu George “Lister” Sabuni ambaye aliweza kumpa maelekezo ya nini cha kufanya kwenye mpambano huo wa mwaka. 
Katika raundi ya 2, 3 na 4 Segu aliuonyesha umati wa mashabiki wa Thailand kuwa yeye kweli ni bingwa mtarajiwa na hakwenda Thailand kula wali wao ila kuiwakilisha nchi yake ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Segu alimhenyesha Pathompothong vilivyo kwa kumchakaza kwa makondde mfululizo hususan akiutumia mkono wake hatari wa kulia ambao ulionekana dhahiri kuwa unaleta madhara makubwa kwa Pathompothong. 

 Ilididi timu ya wataalam wa Pathompothong kutafakari namna ya kumdhibiti kijana huyo wa Kitanzania ambaye kweli alionekana kuwa alienda Thailand kuuchukua mkanda wa IBF Pan Pacific na sio kufuata ulaji! Raudi ta 5 Pathompothong aliingia ulingoni akiwa mtu tofauti kabisa akirusha msumbwi mfululizo na kutembea ulingoni kama siafu huku akimvuta Segu kwenye kamba ili amkandamizie masumbwi yake. 
Kijana huyo nadhifu wa kitanzania (mwenye sura nzuri ya kuvutia na ambaye wasichana wengi wa Thailand walishinda karibu na hoteli aliyoshukia ili kuweza kuongea naye) alitumia wakati huo kumwonyesha Pathompothong kuwa yeye hababaishwi na masumbwi yake kwani amefanya mazoezi ya kutosha. 
Segu alibadilishana masumbi na Pathompothong vilivyo na kuufanya umati wa mashabiki waliojazana kwenye ukumbi huo kumshangilia kama vile yeye ndiye bondia wao wakiimba Tanzania, Tanzania, Tanzania! Katika raundi ya 6 mabondia wote waliingia ulingoni kama vifaru na kubadilishana masumbwi ya mchanganyiko (combinations) wakitafuta kudhibiti harakati za mpinzani mwenza. 

Ni katika kubadilishana huku kwa masumbwi ambako Segu aliumizwa mkono na Mthailand Pathompothong. Inawezekana kuwa ni katika juhudi za kumzuia ili asiendelee kurusha masubwi ya nguvu na kudhoofisha nguvu zake. 
 Kuumia mkono kwa Segu ilikuwa dhahiri kwani mwanzoni mwa raundi ya saba wakati Pathompothong alipokuwa anamiliki ulingo dhidi ya kijana huyo mtanashati wa kitanzania. Katikati ya raundi ya saba Segu aliona kuwa hawezi kuutumia mkono wake vizuri na kumwashiria refarii wa mpambano kuwa anaacha! 
 Segu aliacha pambano hilo katika raundi ya saba wakati mashabiki wengi katika ukumbi huo wakiwa wanaimba Tanzania, Tanzania, Tanzania kwa jinsi alivyokuwa anapeperusha vyema bendera ya “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ndiyo maana Watanzania tunaogopwa kwa maneno mengi.Hivi Ushindi huwa unahesabika wakati gani kwenye ulingo wa Ngumi?Badala ya kueleza kwa ufupi,Segu kashindwa raundi ya xxx japo kajitahidi,unaaanza maneno mengi bila kusema ukweli.

    TUBADIRIKE,HIZO NI SIFA ZISIZO NA MEDALI.

    ReplyDelete
  2. Watanzania ndiyo maana tunaogopwa kwa baadhi ya nchi za wenzetu na hata Wazungu walishatujua tuna maneno mengi matamu sana na huku ukweli na uongo vyote tukiviremba kama uweli.

    Kwani kwenye ulingo wa ngumi,ushindi hupatikana wakati gani?Na nini kina mpatia mtu ushindi?Mtu anaeleza hadidhi ndeeefu kana kwamba Segu kashinda.
    Eleza kwa ufupi,katolewa round ya ngapi na kajitahidi sana basi.

    Aibu,kweli.TUBADIRIKE NA TUENDE NA WAKATI.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2013

    kapigwa mbona tunaanza maneno mengi eti ameumizwa??

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2013

    NANI MKWELI?

    http://www.boxingnews24.com/2013/05/pathompothong-defeats-segu-in-impressive-performance/

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2013

    Nikweli hata mie sikubali aina hii ya utoaji taarifa.Habari ndefu lakini haina kicha wala miguu.Waandishi wetu wabadirike, nakumbuka hata pambano la cheka ujerumani waliandika uzushi hivihivi eti mwanzoni mwa pambano cheka alionekanakumdhibiti mpinzani wake vizuri, baadae inasemekana kuna mtu aliibuka toka kona ya ulingo upande wa cheka na kutoa ishara ya kusimamisha pambano hivyo cheka akapoteza pambano.NIvizuri kuwa wawazi ili kama kuna makosa yarekebishe, nafahamu umuhimu wa uzalendo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...