Na Abdulaziz Video,Lindi
Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali
za mitaa [TAMISEMI] Mhe Kassim Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa
amewataka wanasiasa mkoani Lindi kuacha tabia ya kuwa chanzo cha
kuchochea vurugu katika jamii badala yake washirikiane na watendaji na
wananchi ili kuinua mkoa huo ambao huko nyuma kimaendeleo.
Naibu waziri huyo ametoa wito huo wakati alipokuwa anazungumza na
wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri mkoa [RCC] katika ukumbi wa
mkuu wa mkoa Lindi.
Alisema kazi kubwa ya wanasiasa ni kutembelea wananchi kwa lengo la
kuwasikiliza kero zao ,kuwahimiza na kuwahamasisha wananchi katika
maeneo yao ili kuchochea maendeleo na sio kuchochea kufanya vurugu na
kusababisha kuvunjika kwa amani.
"Wanasiasa wamekuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika
maeneo yao kwa kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo
badala ya kushiriki vurugu.
“Sio vyema wanasiasa waliochaguliwa na wananchi kwa ajili ya kusimamia na kuwawakilisha wakatumia nafasi hiyo majukwaani kutamka maneno ya uchochezi na kusababisha kupotea mwelekeo wa kuwaletea wananchi wake maendeleo hii inaonesha usivyotosha kwa wapiga kura", alimalizia Mhe Majaliwa
Wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Lindi wasikiliza kwa makini kikao cha Bodi ya Barabara
Wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Lindi wasikiliza kwa makini kikao cha Bodi ya Barabara
Naibu Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa ambae Pia ni ,Mbunge wa jimbo la Ruangwa, Mhe Kassim Majaliwa, akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dkt. Nassor Ally Hamid wakati wa mapumziko mafupi ya Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mhe Ludovick Mwananzila akifunga kikao cha bodi ya Barabara Mkoa


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...