Benki ya NMB imemkaribisha mshindi wa milioni 100 wa Vodacom MAHELA , Bwana Valerian Nickodemus kwa kumfungulia akaunti na kujitolea kumpa mafunzo ya ujasiriamali na matumizi sahihi ya fedha ili kumwezesha kuwa na matumizi yenye tija katika maisha yake.

Mshindi wa shilingi Milioni 100 katika promosheni ya Vodacom MAHELA, Bw. Valerian Nickodemus (kati) akifurahi pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkuu wa chapa na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twisa baada ya kukabidhiwa fedha hizo.

Mshindi wa shilingi Milioni 100 katika promosheni ya Vodacom MAHELA, Bw. Valerian Nickodemus (kati) akikabidhiwa kadi yake ya NMB ATM na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kulia) baada ya kufungua akaunti katika benki ya NMB. Akishuhudia ni Mkuu wa Chapa na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twisa.

Mshindi wa shilingi Milioni 100 katika promosheni ya Vodacom MAHELA, Bw. Valerian Nickodemus(kati) akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kulia) baada ya kukabidhiwa kadi yake ya NMB ATM, akishuhudia ni Mkuu wa Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2013

    Vipi usalama wa kijana huyu, kwamba kila mmoja ajua kuwa ana akaunti NMB ya milioni 100?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2013

    Ushauri wa bure.....nunua viwanja jenga nyumba za kupangisha!...hautopata presha na utaendelea kula taratibu kila mwezi

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2013

    Hivi bongo bahati na sibu haina kodi? Maana hapa ughaibuni kasali kwenye kila transaction lazima apate pande lake na pande la bahati na sibu ni percent kubwa sana, si swali tu la kiungwana
    Asanteni,
    Mdau usa

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2013

    Labda Marekani, lakini Canada hamna kodi katika bahati nasibu na kila wiki watu wanashinda milioni nne dola hapa (sio za korosho).

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2013

    Ohhh Mwenyezi amemwona Kijana.

    Hayo ndio mafao yake ya uzeeni!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2013

    Heko Bwana Mdogo,

    Omba upate mke mwema pia zaidi ya neema iliyokushukia.

    Pana msemo wa Wamagharibi usemao ''when you see a successful man a careful woman is on the left soulder'',,,YAANI ''umwonapo mtu aliye fanikiwa mwanamke makini yupo bega lake la kushoto''


    USEMI huo pia una KINYUME CHAKE LICHA YA KUWA UMETOLEWA KWA UPANDE MMOJA ni ya kuwa ''when you see a suffering man probably it might be a case of someone woman on his left shoulder'' YAANI ''umwonapo mtu amekwama yawezekana maesababishiwa na mwanamke Fulani pembeni yake''

    HIVYO DAIMA OMBA UPATE MKE MWEMA!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2013

    vp kijana huyo ndugu yangu kelvin twisa hajakupiga mzinga kweli??maana nijuavyo bongo mtu kukusindikiza kwenye hatua zote hizo za kufungua account lazima mwisho wa siku akuombe hela ya chai...na kwa mahela yote hayo hela ya chai si chini ya 1milion..!

    mdau
    texas

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2013

    Hapa UK, ukishinda pesa kwenye bahati nasibu hulipi kodi!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2013

    Haya kijana, zamani zile tukisema "zali limekuangukia msela nondo". Itunze pesa ikutunze,

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2013

    Duhhh hivyo kumbe Marekani Majanga sana?

    Yaani KODI yao wanakaba lika kona kama Bongo?

    Maana Bongo msala wa Kodi, yaani ukikaa vibaya ukashindwa kutoa Hoja Maafisa wa Kodi wanaweza kukusumbua hata kama Biashara haijafanyika wakataka uwape chochote!

    Kanuni za KODI Dunia nzima ni kuwa INALIPWA KWA KILA BIASHARA INAPOFANYIKA, HIVYO KAMA HUKUFANYA BIASHARA NA HAKUNA USHAHIDI HUSTAHILI KULIPIOSHWA KODI.

    KINYUME NA HAPO KAMA UTALAZIMISHWA KULIPA KODI HUKU BIASHARA HUKUFANYA YAANI 'NO SHOW' INAKUWA NI TAX REGIME, OR DESCRIMINATIVE TAX SYSTEM NA SIO FRIENDLY TAXATION SYSTEMS!

    SASA HAPA (kwenye pointi za juu) NDIO MAAFISA WA KODI WASIO WAAMINIFU BONGO WANAPOPATIA UWEZO WA KUNUNUA MAGARI NA KUJENGA MAJUMBA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...