Mtanzania na Mkenya waliingia supermarket moja jijini London, walipotoka Mkenya akawa anajigamba kwamba wakenya ni wajanja kuliko wa Tz huku akimwonyesha mTz chocolate 3 alizoiba supermarket, mTz akamshawishi warudi tena ili na yeye akamwonyeshe ustadi wake. 

walipofika ndani MTz akamwambia mhudumu nataka nikuoneshe mazingaombwe, hebu niletee chocolate tatu, yule mhudumu akazileta, jamaa akazila zote mbele ya mhudumu halafu akasema unaona nimekula chocolate tatu lakini amini usiamini chocolate zako zote zipo mfukoni kwa huyu jamaa, mhudumu akamkagua Mkenya mfukoni akachukua chocolate zake zote 3 huku Mkenya akabaki ameduwaa. 

je, nani mjanja kati yao??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2013

    Mtanzania na Mkenya madereva pale London kwa bahati mbaya wakagongana,magari yao yakaharibika ile mbaya,lakini wao wakatoka kwenye accident hiyo salama kabisa.Ndani ya gari ya mtanzania kulikuwa na chupa ya champeni ambayo haikuvunjika,akaifungua na kumpa glasi mkenya, cheers.Baada ya dakika hivi mkenya akamuuliza mtanzania, mbona wewe hunywi?Akajibiwa, nitakunywa, lakini kwanza nangojea traffic wafike.(Samahani original joke)

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2013

    HAHAHAHAHAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2013

    wote wezi hakuna mjanja; mtaenda kujibia.

    Inabidi ule unachotolea jasho ndiyo ujanja; nje ya hapo si ujanja.

    Kwa hiyo hakuna mjanja kati yenu ninyi; yani si mtz wala mkenya;

    wote mukajifunze kutoa jasho kupata hitajio na si vinginevyo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2013

    Hakuna mjanja hapo, mmoja mwizi na mwingine anaona noma kupelekana polisi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2013

    Mtz funiko!

    Pana sehemu kama Burundi Mtz hapandishwi Kizimbani Mahakamani kwa kuwa anajua sana kujieleza ni lazima atashinda Kesi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2013

    Si mchezo wizi ni Kipaji!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2013

    Ingine ya ujanja wa aina yake,

    Msomali mmoja alikuwa Mpakani Namanga lakini upande wa Tanzania, akawa na Lori na Tela lake.

    Lori lilikuwa na namba za usajili za Tanzania, wakati Tela lilikuwa na namba za usajili za Kenya.

    Msomali akapigiwa simu ya kuwa afunge Tela aendeshe kwenda Arusha, kwakuwa Tela la Lori lake lipo huko na Kichwa cha Tela la Kenya kipo Arusha.

    Ile Msomali anaingia mjini Arusha akasimamishwa na Trafiki akaulizwa je inakuwa Lori ni la TZ na TELA la Kenya uedneshe?

    Msomali akajibu ''Shio aajabu Kichwa Tansania nakaribisha kutembesha Mkia Kenya''

    akisema KICHWA CHA TANZANIA KINAUKARIBISHA KUUTEMBEZA MKIA WA KENYA!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2013

    Mtanzania mjanja mana mkenya hawezi kwenda kushtaki popote kwa kuwa hakuzilipia chocolate na zimerudi tena dukani! Akili ni nywele kila mtu ana zake.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2013

    Hm. Aliyesema wizi ni kipaji noma!!!

    Ila watanzania ulimwengu mzima wanasifika kwa wizi na utapeli ila siyo wajanja. maana wanaiba na wanakamatwa. Ila kuna badhi ya maeneo kwenye inchi jirani ambako watanzania ikifika mida ya jioni hawasogelewi kwa kusemekana hawaachi kitu,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...