Na Francis Godwin wa Matukio Daima Blog,Iringa
SAKATA la vurugu za machinga na polisi mjini Iringa limechukua sura mpya baada ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kumfikisha mahakamani mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa pamoja na watuhumiwa wengine zaidi ya 70
Huku mahakama hiyo ikitoa masharti nafuu ya dhamana kwa watuhumiwa hao na kuwaonya kutofanya kosa kwa kipindi chote cha kesi hiyo inapoendelea kusikilizwa .
Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Godfrey Isaya leo majira ya saa 8 mchana huku wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa na msafara wa magari zaidi ya matatu likiwemo gari ya maji ya kuwasha .
Mbali ya mbunge Msigwa kupanda gari ndogo ya wazi ya polisi pamoja na watuhumiwa wawili wanawake waliokamatwa katika vurugu hizo bado watuhumiwa wengine zaidi ya 70 walitumia usafiri wa karandinga la polisi.
Mbele ya mahakama hiyo wakili wa serikali Adolph Maganda alisema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja wanatuhumiwa kwa makosa matatu likiwemo la kushiriki mkutano na kufanya vurugu ,uchochezi na kuharibu mali kinyume na sheria .
Huku mbunge akisomewa mashitaka mawili likiwemo kushawishi na kufanya mkutano bila kibali .
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao huku wakili wa serikali akidai kuwa hana pingamizi na dhamana kwa watuhumiwa hao wote ,hata hivyo wote wamekana mashitaka yote yaliyotolewa dhidi yao.
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao huku wakili wa serikali akidai kuwa hana pingamizi na dhamana kwa watuhumiwa hao wote ,hata hivyo wote wamekana mashitaka yote yaliyotolewa dhidi yao.
Hata hivyo makimu anayesikiliza kesi hiyo alisema kuwa dhamana kwa washitakiwa wote ipo wazi kwa kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika pamoja na kusaini hati ya dhamana ya Tsh milioni moja .
Hadi majira ya saa 10 jioni mahakama hiyo ilikuwa ikiendelea na mchakato wa kupitia barua za dhamana kwa wadhamini huku mbunge akiwa wa kwanza kudhaminiwa ,mbali ya mbunge watuhumiwa kati ya 74 waliokuwa bado kupata wadhamnini ni watuhumiwa sita pekee.
Katibu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonakulima alisema kuwa mchakato wa kuwadhamini watuhumiwa wote waliosalia unaendelea kufanyika na kuwa wana uhakika wa watuhumiwa wote kudhaminiwa .
Hadi majira haya ya saa 10 .40 jioni wakati habari hii inakwenda mitamboni bado mahakama ilikuwa ikiendelea na umati wa wafuasi wa Chadema ukiwa nje ya mahakama hiyo kusubiri watuhumiwa hao kudhaminiwa .
Wakati huo huo wananachi waliofika mahakamani hapo kushuhudia mbunge wao akifikishwa mahakamani wamempongeza mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Iringa (FFU) Said Abdulah Mnunka kwa kusimamia amani na utulivu katika eneo hilo la mahakama na jinsi ambavyo alivyoweza kupambana na machinga pasipo kumwaga damu kwa siku ya jana wakati wa vurugu hizo


Tuzidi mambo ya kuiga nje ya nchi, wabunge kutolewa ndani ya bunge kwa nguvu, wabunge kurushiana ngumi katika bunge, wabunge kukashifiana na kuzuliana uongo ndani ya bunge na katika vyombo vya habari, wabunge kupinga amri za serikali na za polis, askari kukamata ovyo ovyo wabunge na wananchi na kupoteza muda mrefu kufungua kesi ambazo mwishowe watuhumiwa huachiliwa huru. hongera watanzania wenzangu!!!!!!
ReplyDeleteKama walinzi wa amani ya nchi wanakuwa waoga kiasi hiki wananchi mnategemea nini?. Polisi kutumia nguvu kupita kiasi ni woga huo. Polisi wapelekwe shule wafundishwe namna ya kufanya kazi zao. Hawana elimu hawa, hawana nidhamu hawa n.k Wanafanya kazi kuganga njaa tu. Serikali iliangalie hili vinginevyo nchi itajikuta ya hovyo
ReplyDelete