Mfalme wa muziki wa asili nchini Costa siboka 'Mfalme' anatarajia kuanza ziara yake ya utambulisho wa nyimbo mpya hivi karibuni.Siboka wiki ijayo atakuwa jiji la Mwanza na kuzunguka visiwa vyake vyote vinavyozunguka jiji hilo.Ikiwemo visiwa vya ukerewe,kisiwa cha ukara,kisiwa cha Ghana na kumalizia mjini Geita.
Baada ya hapo ataelekea Mjini Mbeya na Tunduma kwa ajili ya kutambulisha nyimbo mpya inayoitwa TWISILE aloimba kwa Lugha ya kinyakyusa.Siboka Mfalme anadhaminiwa na KONYAGI, CXC Africa na Michuzi Blog.
Vilevile ameanza muziki huu wa asili kwa kudhaminiwa na Balimi Extra Lager. Siboka anaomba wadhamini wengine wajitokeze kumpiga tafu. Halikadhalika, anasema Mfalme Siboka,  katika ziara hiyo atatangaza AMANI kwa Watanzania wote.
 Juu na chini ni Siboka Mfalme akiwa katika zaiara za mikoani siku za nyuma


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...