Mmoja wa wananchi
wanaoshiriki katika ulinzi wa Pori la Akiba la Selou akingoa jino la
Tembo aliyeuawa na majangili na kisha kukurupushwa na askari wanyama
pori kabla hajafanikisha mpango wake wa kuchukua meno ya tembo huyu.
Wadau wa wanyamapori wanabashiri kuwa hivi sasa idadi ya tembo wanauawa
kwa ujangili ni kubwa mno kiasi cha kuhatarisha uwepo wa wanyama hao
katika kipindi kifupi kijacho endapo hatua za kukabiliana na ujangili
hazitachukuliwa haraka na kwa nguvu kubwa.
Meno ya Tembo
yaliyokutwa yakiungua kwa moto baada ya watu wanaosadikiwa kuwa
majangili kukurupushwa na askari wanyama pori wakati wakijiandaa
kukamilisha zoezi la kukausha meno hayo ili yasafishwe kwenda sokoni
Sehemu ya Pori la Akiba
la Selou ambalo kwa sasa linakabliwa na chngamoto kubwa ya kukithiri kwa
vitendo vya ujangili unaotishia kutoweka kwa wanyama hasa tembo.
Wakati Tembo wakiwa
hatarini kutoweka kutokana na ujangili wanyama wengine wanaendelea
kupeta akiwemo ngiri huyu ambaye ni mzee. hatari anayokabiliana nayo ni
ya kuliwa na simba, chui, duma na wakati mwingine mbwa mwitu. hata hivyo
wataalamu wa wanyamapori wanasema wanyama kama ngiri ni halali kuliwa
kwa sababu wapo porini pamoja na umuhimu wao pia ni chakula kwa wanyama
walao nyama.
Pundamilia nao mambo yao poa huko porini.





Huyo ngiri hapo juu ni kitowewo halali kabisa kwa mwanadamu, ukiaondoa ndugu zetu wa kiislamu..na huyo ngiri mpaka kafikia uzee huo na kashikashi ya wanyama wanaotaka kumla basi kweli ni shujaa sanaaaa...maana nadhani atakuwa na rekodi ya mapambano makubwa ya simba, chui, duma, mlafi fisi na wanyama wenginine wala nyama....sikitiko liko kwa hao tembo tu....serekali fanyeni kweli...
ReplyDeleteHakuna mwenye ubavu wa kumkamata ngiri kati ya hao uliwataja, labda huyo ngiri awe mtoto!
ReplyDeleteni serikali ndio ya kulaumiwa endapo tembo wetu watateketea kutokana na ujangili.Wenzetu wa Kenya na hata hata afrika kusini hawalali usingizi kwa kufikiria namna ya kulinda rasilimali hii muhimu.Vifaa kama helikopta zana zingine vimenunuliwa ili kupigana na majangili. Lakini kwetu huwezi sikia hilo.Inasikitisha sana. Sasa hivi tunakaribisha mpaka wachina ili waje kuwekeza kwenye mbuga za wanyama!!!Tunategemea nini hapo?? Hivi viongozi wetu huwa wanafikiria nini?? Kwa mwenendo huu ikifika miaka kumi ijayo hatutakuwa na tembo wala faru kwenye hifadhi ya Selou. Nawasilisha.
ReplyDeleteyaani kati ya wanyama wote waliotajwa hapo hawawezi kumkamata hata "ngiri mzee"? labda ngiri mtoto? basi hao wanyama watakuwa mashoga.
ReplyDeleteTunahitajika kuwahami Tembo kuangamia kwa njia ya KIDIJITALI!
ReplyDeleteKama tunao uwezo wa kuimarisha Mabenki na Ofisi nyeti kwa kutumia udhibiti wa Kidijitali kwa nini maeneo waliyopo tembo yasiwekwe electronic fences zinazo detect nyendo za Viumbe wanaofika hapo sambamba na kuwafunga electronic badges Tembo wote na Faru wanaohesabika kwa idadi yao sasa.
Mpango uwe hivi:
Iitishwe Tender Notioce ya kuwatafuta Bidders watakaotoa ''Electronic control for selected Species of wildlife, on management''
FILD TASK:
1.Kuestablic Wildlife Management center Electronic Circuit, hapa ndio Makao ya Kituo cha usimamizi.
2.Kufunga electronic systems na kuzungusha detecting fence ktk eneo waliopo Tembo na Faru.
3.Kuwafunga Detected Electronic Badges Tembo na Faru kwa idadi na namba maalum za utambuzi.
4.Watalii watafungwa ELECTRONIC BADGES maalum za utambulishi wakiingia eneo hilo.
5.Wasimamizi na Watumishi wa Mamlaka ya Wanyama Pori watakuwa na Electronic Badges zao za Utambulishi.
Atakaye onekana au kuwa detected ktk Etecronic system atakuwa ndio JANGILI!!
Nadhani kwa njia ya DIJITALI ndio tutamudu Jukumu hili licha yachangamoto zilizopo.
HAKUNA KINACHOSHINDIKANA CHINI YA JUA LABDA IWE KIFO TU KINACHOPANGWA NA MWENYEZI!