Na Mzalendo Albert, Arusha
Alichokisema Rais Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa kutafuta amani nchini DRC hakina ubaya wowote, kupelekea Wanyanrwanda wamjie juu na kuanza kumshambulia kwa lugha ambazo hazina ustaarabu kutokana na matamshi yake ya kutaka amani ipatikane kwa mazungumzo. Pengine kwa kuanza nielezee kwa ufupi alichosema Rais Kikwete ambacho kimesababisha Wanyarwanda wanatahamaki kiasi hiki.
Ajenda ya mkutano ilikuwa ni juhudi za kutafuta amani nchini DRC. Inaeleweka kwamba vikundi vingi vya waasi kutoka nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu vinafanya shughuli zake kutokea DRC. Vikundi hivyo kwa miaka mingi vimekuwa viki destabilize DRC kwakuwa muda mwingi vimekuwa vikiendesha mapigano ndani ya Congo. Juhudi za kuvisambaratisha vikundi hivyo kwa njia za mapigano hazijazaa matunda kwa zaidi ya miaka 19 sasa.
Miaka yote, Tanzania imekuwa ni kimbilio la wanyonge Barani Afrika. harakati za ukombozi wa nchi zote kusini mwa Afrika zimefanyikia Tanzania. Aidha, Tanzania kwa miaka mingi imefanya juhudi za kutafuta amani sio nchini Congo peke yake, bali katika eneo lote la ukanda wa maziwa makuu. Mengi yamefanywa ikiwa ni pamoja na:
1) kuwa msuluhishi katika mazungumzo ya kutafuta amani Rwanda, Burundi
2) Kuwa mwenyeji wa wakimbizi kutoka Rwanda, Burundi, DRC
3) Kupeleka majeshi ya kulinda amani
Kitu kumoja ambacho Tanzania imejifunza katika miaka yote hii, ni kwamba mapigano/vita mara nyingi sio suluhu ya kudumu ya kumaliza uhasama. Mazungumzo ndio njia bora yenye kuweza kuleta maridhiano.
Ipo mifano mingi ya matunda ya mazungumzo. Leo hii kikundi kilichokuwa kinajulikana kuwa ni cha kigaidi nchini Burundi FNL, ni sehemu ya Serikali ya Burundi kwa sababu, wote walitoa nafasi ya mazungumzo.
Vikundi vingi vya kigaidi vya DRC, viligeuka kuwa vyama vya siasa na kushiriki kwenye uchaguzi, kwa sababu vilikubali mazungumzo.
Leo hii DRC inafanya mazungumzo na vikundi vya waasi na vya kigaidi nchini Uganda ili kutafuta suluhu. Mazungumzo haya yametokana na juhudi za wakuu wa nchi za maziwa makuu ambayo Rwanda ni mjumbe. Hivi nani asiyejua jinsi gani vikundi hivyo vilivyofanya vitendo vya unyama na mauaji kwa wananchi wasio na hatia? Wameua, wamebaka, wameiba.....wamefanya kila jambo hovu, lakini bado imeonekana busara ya kukaa mezani kuzungumza.
Ukiachilia mifano ya kwenye ukanda huu, ipo mifano mingine mingi tu nje ya ukanda.
Nothern Ireland
Yaliyotokea Ireland ya kaskazini kila mtu anafahamu. Maelfu ya watu waliuawa kutokana na vitendo vya kigaidi vya IRA. Lakini mwisho wa yote, Serikali ilikaa nao meza moja, matokeo yake ni amani kupatikana Nothern Irrland.
Msumbiji na Angola
Huko Msumbiji nani asiyekumbuka magaidi wa Renamo walivyoua maelfu ya watu nchini humo. Lakini mwishowe walikaa mezani na Frelimo, amani ikapatokana. Hata Angola, nani asiyekumbuka Jonas Savimbi alivyoua mamia ya wananchi wasio na hatia.
ANC na apartheid
Huko Afrika ya kusini nani asiyejua kwamba maelfu ya watu walipoteza maisha yao kutokana na sera za ubaguzi na manyanyaso ya serikali ya makaburu. Lakini baada ya kuitikia wito wa kuzungumza, leo hii wanaendelea kuishi kama taifa moja.
Wayahudi na wajerumani
Pengine mifano niliyoitoa waweza kusema haifanani na Rwanda,kwa kuwa nchi zile haziku experience mauaji ya kimbari. Lakini huko Ujerumani, mauaji makubwa yalifanyika dhidi ya Wayahudi. Kila mtu anafahamu hilo. Lakini leo hii ndugu wale hawaendelezi uhasama....
Baada ya mifano hiyo, ni dhahiri kabisa kwamba alichoshauri Rais Kikwete ni sahihi kabisa. Nchi zote za maziwa makuu ambazo zina vikundi vinavyohasimiana navyo, watumie njia ya mazungumzo kama njia bora ya kumaliza uhasama na kutoa fursa kwa wahusika waondoke Congo na kurejea nchini mwao.
Kwa kesi ya Rwanda...sio kweli kwamba kila mwanachama wa FDLR alihusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Wapo wana FDRL ambao walizaliwa baada ya 1994 na wanaishi uhamishoni ikiwa ni pamoja na DRC.
Hivi ni haki kuwajumisha hao kwenye kundi la magaidi waliofanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994?
Je hatuoni kutoa fursa ya mazungumzo itawawezesha wana FDLR ambao hawakuwa na hatia na wala hawakuwepo mwaka 1994 kupata fursa ya kurejea nchini mwao?
Na je Rwanda haioni busara ya kutumia njia ya mazungumzo itawezesha kufikia makubaliano na waasi hao wawatoe waliohusika na mauaji ya kimbari wakashitakiwe?
Kufanya mazungumzo hakumaanishi ni kutoa msamaha, la hasha. Kufanya mazungumzo ni kuweka mazingira ya kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na kuweka misingi ya kuchukua hatua mbalimbali kwa wahusika.
Wanyarwanda wame overreact na kuwa emotional pasipo kuwa na sababu ya msingi. Rais Kikwete na watanzania kwa ujumla, ni watu wa mwisho kuwa sympathiser wa wanachama wa FDLR waliohusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994 na wale wanaoendeleza mapigano hivi sasa huko DRC kwani athari za vitendo vyao vilitugharimu sana.... kwani sio tu vilikiuka misingi ya utu ambayo Tanzania inaiheshimu na kuipigania siku zote, bali pia ilitugharimu kwa kupokea wakimbizi katika vipindi tofauti. Vitendo vyao bado vinaendelea kutugharimu hadi leo. Uwepo wa majeshi ya Tanzania kulinda amani nchini DRC ni matokeo ya vikundi vya aina ya FDLR kuvuruga amani nchini DRC.
Ikumbukwe pia Kitendo cha Tanzamia kuwa Mwenyeji wa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbari ICTR, ni ushahidi tosha wa namna ambavyo Tanzania haiungi mkono mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda, haina huruma kwa wale wote walooshiriki katika mauaji ya kimbari.
Hivyo, hapa kama kuna mtu wa kuomba radhi, ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na wanyarwanda wengine wote walio over-react na kumshambulia Rais Kikwete.
Kusoma walivyomsema Rais Kikwete BOFYA HAPA
Ikumbukwe pia Kitendo cha Tanzamia kuwa Mwenyeji wa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbari ICTR, ni ushahidi tosha wa namna ambavyo Tanzania haiungi mkono mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda, haina huruma kwa wale wote walooshiriki katika mauaji ya kimbari.
Hivyo, hapa kama kuna mtu wa kuomba radhi, ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na wanyarwanda wengine wote walio over-react na kumshambulia Rais Kikwete.
Kusoma walivyomsema Rais Kikwete BOFYA HAPA


Kama ilivyo desturi yetu watanzania hututojiingiza katika malumbano nao. Tutaacha busara itawale katika hili. Ni kuwaacha tu wao wamimine maneno kama watakavyo (mara enemy # 1, sympasizer, traitor n.k.)sie hatutalumbana nao. Bado tutawahesabu kama jirani,iwe isiwe. Na majirani wapo wa aina nyingi kama nyote mjuavyo. Tusemeni mtakavyo lakini sisi bado tutawapenda tu kama jirani zetu.
ReplyDeletewaacheni wapige kelele washazoea kuuwana kama kuku hao hawana ubongo mzuri na wakileta mdomo mrefu haki ya nani tutawamaliza na kuigawa rwanda kuwa mkoa wa tanzania
ReplyDeletetumewasaidia kwa muda mrefu sana kupokea wakimbizi wao na sasa wanaanza ujeuri wataishia kumalizana wenyewe kwa wenyewe kwetu hawampati mtu
wivu wao wote unatokana na kuona nchi yetu tunaishi kwa amani upendo na ushirikiano hata wanapotuona sisi huku ughaibuni wanaumia roho sana maana wanatuonea wivu watanzania tunavyopendana na kushirikiana
kwa uwezo wa mungu tanzania tutabaki kuwa na amani na upendo na tutamfanyia kazi kila atakaejaribu kuvuruga amani ya nchi yetu
chonde chonde watanzania wenzangu mnaona jinsi majirani wanavyotuonea wivu wa amani mpaka wanaanza kutufatafata wengine wameanza na kesi ya ziwa nyasa
na bado mtaumia sana na siku chache zijazo mzee mzima obama ndania ya nyumba kubwa ya white house dar es salaam
hebu tupisheni tupumue na mivita yenu huko alaaaa $%#^&* zenu
Watani zetu wajadi nao walibishia J.k alipotoa comment kuhusu mwelekeo wa sias zao kutokuwa sawa. Lakini badala yakufanyia kazi ile comment walianza ulalamishi, uliza waliyakuta watu kuchinjana. Wacha huyo Kgm atoke madarakani kama hatachinjana tena huko Rwanda. Badala ya kupwayuka hayo maneno yao, wangetulia na kutafakari, anayekuambia ukweli ndiyo rafiki. Sasa hao majambazi yao yanaiharibu nchi ya jirani DRC. JK namsifu katika hilo kwa kuusema ukweli kwakuwa DRC na watu wake wanachelewa maendeleo kwakua na vikundi kutoka nchi za Rwanda na Uganda kuleta shida huko. Ukweli utasimama daima hatakama wakaleta fedhuli lakini siku moja mtakumbuka, asiye ziba ufa atajenga ukuta.
ReplyDeleteIli amani ipatikane katika Great Lacs Region ni lazima Rwanda ikae na hao waasi wao wa FDLR wamalize migogoro yao,mbona DRC inazungumza na M23,kwa nini Rwanda ikatea? Inaonyesha Wanyarwanda hawataki maendeleo ya Bara la Afrika.
ReplyDeleteNaunga mkono Mh. Jakaya Kikwete kwa kutoa wazo nzuri hilo la busara.
Janga la wakimbizi ni Tanzania ndio inahadhirika kila mara.
Naona hamjawaelewa Wanyarwanda. Wanachotaka ni kuona waasi wanakuwa sehemu ya DRC na sio kurudishwa Rwanda. Wanachodai ni kwamba hao waasi wameishi DRC kwa miaka 19 kwa sababu hiyo wanaona kama wanastahili kuwa raia wa DRC na sio Rwanda? Unaposema wakae waongee ulitarajia waongee nini wakati wao msimamo wao ndio huo? Wao wanaona naturalisation ya waasi nchini DRC inawezekena ila Tz ndiyo inataka kutibua.
ReplyDeleteKumbukeni Rwanda ina shida ya Ardhi ndio maana wanapopata fursa kama hiyo wanaitumia vilivyo. Hata walikasirika walipoona mnawarudisha watu wao waliokimbilia Tz wakati wa vita yao. Wangependa wabaki huku Tz.
Ardhi ndiyo inawafanya hata wamchukie Kikwete na Watanzania wote kwani walitaka kutumia mgongo wa EAC kuingia na kumiliki Ardhi Tanzania na JK akawawekea ngumu.
Mheshimiwa tuambie vijana wako kama kuna joka tuko tayari.
ReplyDeleteEh, hii hotuba imewashangaza Wanyarwanda eti waongee na magaidi wa FDLR, watu ambao walisababisha mauaji ya kimbari. Wanaona kama JK kapoteza muelekeo kabisa na wengine wanadai awatakie radhi Wanyarwanda.
ReplyDeleteHili sakata halijaishia hapa kwa kweli, lakini mimi binafsi sioni kama kuna ubaya wowote na sidhani JK ameshauri wakae chini - alichosema ni labda imefikia wakati mzuri hawa magaidi walio pembezoni waitwe na washirikishwe katika kutatua swala hili la DRC mashariki. Na sidhani kama ni kitu kibaya kwani pia ni Tanzania tuu katika EAC iliyopeleka wanajeshi wa kulinda amani, sasa watu wanataka vijana wetu tuu wafe katika limgogoro ambalo halituhusu wa Tanzania?
I read President Jakaya Kikwete comments and frankly don’t find them offensive, some of my friends from Rwanda agree with me as well. Not a journalistic critic rather personal from a source that seems to harbor deep and negative feelings against the president of Tanzania. As much as I don’t agree with Jakaya on most of his policies the article seeks to belittle him and Tanzania which has been a pillar and a place of hope to our brothers and sisters from neighboring countries including Rwanda. If one goes in the border cities of Tanzania such as Kagera, Kigoma or even further in like Mwanza, you’ll see many Hutus and Tutsi’s that have been leaving there for years without being profiled or persecuted. I do agree Tanzania like any other country is going through some religious and identity challenges that other countries seek to explore for their own advantages. Frankly she is still in a pretty good shape considering huge populations of Christians and Muslims that consider themselves Tanzanians before their tribes or religions. These challenges existed in the past and few bad apples will always be there, however, Tanzanians will for peace and unity will never be shaken so don’t be fooled. it’s a unique country, full of love, welcomes citizens of other nations with open arms. Tanzanians might disagree with President Paul Kagame and criticize him with respect understanding that regardless of Rwanda’s internal politics his people chose him. There is a sense among many in east Africa that the Rwandan government never wanted Tanzania to participate in the UN peace mission in DRC, is it because they are accused of supporting M23 rebels? Are they doing so? It would have been better to be open than hiding on personal, subliminal and obscured messages. To think Tanzania is or will be isolated is a day dream which will never happen. I hope your views don’t represent the majority of good people of your country that we consider our brothers and sisters.
ReplyDelete
ReplyDeleteninahasira na hivi vijamaa? yaani hiyo taarifa yao imenichefua kwelikweli hata wazamiaji wao waliopo nnchini nawaona kama wadudu.....
Hutu tujitu twa hii region tuna hasira na jeuru chuki bila busara sijui kwa nini.Si kingine hasira zao ziko juu ya JK kuwafurusha M23
ReplyDeleteKwa kweli nimegadhibika sana kama mlivyogadhibika Watanzania wenzangu. Kwa ufupi ule msemo fadhilaka wapundaka ndio naona umetimia!
ReplyDeleteNakubaliana sana na huyu Anyonymous aloandika hivi: ................Naona hamjawaelewa Wanyarwanda. Wanachotaka ni kuona waasi wanakuwa sehemu ya DRC na sio kurudishwa Rwanda. Wanachodai ni kwamba hao waasi wameishi DRC kwa miaka 19 kwa sababu hiyo wanaona kama wanastahili kuwa raia wa DRC na sio Rwanda? Unaposema wakae waongee ulitarajia waongee nini wakati wao msimamo wao ndio huo?...............................
Katika masomo yangu yanayohusiana na Peace and Conflict, naweza kusema hicho ndicho wanachokitaka WanyaRwanda kwa mba ghasia ya FDLR ibaie huko huko DRC na si irudi Rwanda. Tayari kila mtu ameshachukua chake, ardhi na vinginevyo. FDLR wakirudi watadai ardhi na mali za mababu zao, na hapo mzozo utaibuka upya. Ili kuepusha hekaheka hizo, basi wanafunika kombe mwanaharamu apite! Laiti wangezisikia sauti za vilio vya kina mama, watoto na hata kina BABA wanaoogelea kwenye dimbwi la UBAKWAJI (kina baba na mama wote wanabakwa) na kundi hilo la FDLR! Athari ya vitendo hivyo kila mmoja wetu anavijua lakini baya zaidi ni kuvunja ndoa na familia na kuongeza idadi ya watoto wasiokuwa na thamani kwa Wakongo(Hii ni kwa sababu mwanamke anapopata mimba kutokana na kubakwa na mafisadi hao, basi hutengwa na kufukuza ktk familia. Na hata asipofukuzwa akajifungua, mtoto huhesabika kama adui; kwa kuwa amebeba damu ya adui wa DRC) HAli hii inaendelea ktk miji mbalimbali ya DRC!Ni sawa kabisa kwa Kikwete kuwataka hao marafiki wawili kumaliza mzozo huo maana wanakijua vizuri chanzo chake na namna ya kumaliza kadhia hiyo!
kwa jinsi walivyo react inaonyesha ni jinsi gani Rwanda haijawa na amani. vita haitaleta amani
ReplyDeletesuala la pili ni kwamba bila vita (yaani Rwanda kwenda DRC) uchumi wa Rwanda utakufa. kwa hiyo wafikirie amani na watafute njia mbadala za uchumi
Mdau wa 12 hapo juu umenena:
ReplyDeleteSiri ya Mafanikio ya Kiuchumi ya Rwanda ipo nyuma ya Vita ya Mashariki ya Congo DRC,
Inasemekana Utendaji huko Mashariki ya Kongo upo hivi,
1.Wakati vita inapiganiwa, inasemekana Wapiganaji wengine huko Msituni wanakuwa ktk zamu za Uchimbaji wa Madini Migodini, huku wakikusanya Ushuru na Ada ktk barabra zinazopita ktk maeneo wanayoyashikilia.
2.Inasemekana Wafadhili wa vita Mashariki ya Congo DRC wapo ktk miji mikuu ya Rwanda kama Kigali wakijihusisha na Biashara mbalimbali ikiwemo hayo hayo madini.
3.Export base (hasa ya Madini) yanayotoka Rwanda yanatokea Mashariki ya Kongo hapo Rwanda ni kuwa yanapita njia tu.
Hiyo ndio hali halisi, na ndio maana Rwanda inaifanya vita iendelee ili wajiimarishe kiuchumi.
Upatanishaji hajaanza Kikwete!
ReplyDeleteKama mjuavyo Maraisi wetu waliotangulia Hayati Mwl.Nyerere, Mzee Miwnyi na Mzee Mkapa wamekuwa Mihimili ya upatanishi ktk Vipindi vyao vya Uraisi kama hapa chini:
1.KUSINI MWA AFRIKA HARAKATI ZA UKOMBOZI NA USULUHISHI:
1961-1984
Mwl.Nyerere alibeba mzigo mkubwa sana na Tanzania kugharimia ktk masuala haya.
2.MIAKA 1984-1994 MAPIGANO MSUMBIJI, UGANDA, BURUNDI NA RWANDA (Mwanzoni kabla ya Mauaji ya Halaiki ya 1994) Mzee Mwinyi alishiriki ktk usuluhishi.
3.MIGOGORO ZAMBIA, BURUNDI UGANDA NA COMORO, 1995-2004
Mzee Mkapa alishiriki kikamilifu ktk usuluhishi.
4.KUANZIA 2005 HADI LEO HII MACHAFUKO KENYA BAADA YA UCHAGUZI 2007/2008, COMORO,MADAGASCAR,BURUNDI
Mhe.Raisi Kikwete na Mzee Mkapa walichukua jukumu kubwa sana.
Rwanda ninyi ni watoto wadogo sana kwa sisi Wakombozi wa Kusini mwa Afrika TAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA na Mhe. KIKWETE.
Jamhuri ya Rwanda muelewe hivi:
ReplyDeleteLamwe huwezi kupatanisha Upande mmoja huku upande mwingine ukiuacha.
Vita zenu zipo ktk STAILI YA MZUNGU WA NNE (4) YAANI KARATA MOJA INA VICHWA VINATAZAMA MIELEKEO INAYOPISHANA:
1.WALALAMIKAJI(DRC-CONGO)
RWANDA INADAI YA KUWA MAKUNDI YA FDLR NA ADF YANASAIDIWA NA SERIKALI YA KINSHASA DRC-CONGO KUIPIGA NA KUTAKA KUIANGUSHA SERIKALI YA KIGALI-RWANDA.
2.WALALAMIKIWA (RWANDA)
CONGO DRC INALALAMIKA KUWA SERIKALI YA KIGALI-RWANDA INAWASAIDIA M-23 AMBAO WALIKUWA MWANZONI WANAITWA CNDP KUIPIGA DRC-CONGO.
HIVYO NI SAHIHI KUWAYAITA MAKUNDI YOTE KTK MAZUNGUMZO ILI MUAFAKA UPATIKANE NA NDIO SULUHISHO SAHIHI.
KWA SABABU HIYO FDLR NA M-23 WOTE NI WAASI LAKINI WAKAPIGA MIELEKEO TOFAUTI DHIDI YA RWANDA NA CONGO
M-23(ZAMANI CNDP) INAPIGA KUELEKEA DRC-CONGO WAKATI FDRL, NA ADF ZINAPIGA KUELEKEA RWANDA.
HIVYO ILI MUAFAKA UPATIKANE NI LAZIMA ZIKUTANE HIZI:
1-UGANDA,(SERIKALI INAYOSAIDIANA NA SERIKALI YA RWANDA KUIPIGA DRC-CONGO.
2-RWANDA SERIKALI INAYODAIWA KUSAIDIA WAASI WA M-23 KUIPIGA CONGO-DRC.
3-FDRL na ADF MAKUNDI YANAYODAIWA KUSAIDIWA NA CONGO DRC KUIPIGA RWANDA NA KUNDI LA M-23.
4-M-23(ZAMANI CNDP) INAYODAIWA KUSAIDIWA NA RWANDA NA UGANDA KUIPIGA CONGO-DRC NA MAKUNDI YA FDRL NA ADF.
HIVYO KIKWETE NI MWANADIPLOMASIA ALIYEKOMAA KUUTAMBUA UKWELI HUO KTK NO.1 HADI NO.4 HAPO JUU HUKU MZIZI WA VITA UKIWA NI MASLAHI YA KIUCHUMI ZAIDI KTK MADINI YA MASHARIKI YA CONGO.
Jamhuri ya Rwanda ninyi mmetumia muda mwingi kwenye vita za wenyewe kwa wenyewe, ni muda mfupi sana ktk Historia la Taifa lenu mmekuwa na Utulivu (Stability), wakati sisi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumetumia muda mwingi tokea tupate Uhuru mwaka 1961 ktk Vita vya Ukombozi tena wa nchi zingine na Upatanishi huku tukibeba mzigo mkubwa wa Wakimbizi.
ReplyDeleteHivyo Mhe. Kikwete kama Balozi Mwandiplomasia Mwandamizi ameliona hilo!
Mnatakiwa ninyi ndio mumuagize Waziri wenu wa Mambo ya nje Louise Mushikiwabo amwombe radhi Kikwete na Tanzania.
Rwanda mmekuwa mkibebwa sana na kulelewa kwa muda mrefu sana na Jumuiya ya Kimataifa.
ReplyDeleteJe, tutawezaje kuwasuluhisha kama Rwanda mnataka muwe vijogoo na hamtaki kushuka chini?
Je, ninyi ni nani na kwa nini mnataka muwekwe juu wakati tunataka haki itendeke kwa makundi yote?
Raisi Kikwete amewapa ukweli mtupu!
Mhe. Raisi Kikwete ameipiga NGOME KONGWE !
ReplyDeleteJamaa wamekuwa wakiyatumia Mauaji ya Kimbari 1994 kutafuta kubebwa Kimataifa na kweli wameweza kutumia Falsafa ya Mauaji hayo kuwa watu wa kipaumbele zaidi.
Wakafikia kujisahau ya kuwa Dunia inaangalia upande wa pili wa sarafu kwa sababu UN kama ilivyo ina waangalizi ndio wakaona ya kuwa Jamhuri ya Rwanda ina yafuatayo juu ya Vita Mashariki ya Kongo:
(I)Ethnicity,
Kutetea Ututsi kwa kuwa Waasi wa Congo wana unasaba na watutsi wa Rwanda Kihistoria.
(II)History,
Kwa kuwa Hisoria ya unasaba huo unatokana na Watutsi na Manyarwanda walivyo lowea Mashariki ya Kongo na pia ilivyokuwa huko nyuma kipindi cha Ukoloni nafikiri wa Wabelgiji na Wafanransa inasemekana Eneo la Mashariki ya Kongo lilikuwa ndani ya Rwanda (kwa mujibu wa Ramani ya Ukoloni, madai yanayofanana na Malawi juu ya Ziwa Nyasa, na ndio maana ktk moja ya Mikutano na vyombo vya Kimataifa vya Habari Waziri wao wa Mambo ya Nje Louise Mushikiwabo aliwahi kuonyesha Ramani hiyo ikionyesha umiliki huo wa eneo la Mashariki ya Kongo kama sehemu ya Rwanda.
(III)Economy,
Kama Wadau walitangulia hapo juu, Rwanda inavuna madini mengi sana eneo la mashariki ya Kongo, huku Matajiri wa Kitutsi wa madini waliopo Kigali na miji mingine ya Rwanda wakiwa wanunuzi wa madini hayo na wadhamini ya Makundi ya Kivita na Uasi.
HIYO NDIO MBIVU NA MBICHI JUU YA SIASA NA UNDANI WA CHIMBUKO LA VITA VISIVYOISHA VYA MASHARIKI YA KONGO HUKU RWANDA IKITAJWA KWA SAUTI YA JUU KTK VITA HIVYO.
Wanyarwanda-Wakitutsi acheni kujichukulia kama 'very special minority' kitu ambacho kinazidisha mpasuko kati ya Ututsi na Uhutu.
ReplyDeleteMmeishi kwa miongo mingi mkiwa kama wanandugu HUKU CHA AJABU NI KUWA LUGHA YENU NI MOJA!
Hivyo yote ya nini kuhasidiana?
Kagame amefanya mengi Rwanda ya kusifiwa na kuwa kigezo Kimataifa isipokuwa Hesabu hii hapa chini imemshindwa amepata SIFURI:
ReplyDeletedR/dT=(TUTSI)t+(HUTU)t
[JUU NI MGAWANYIKO WA WATUTSI NA WAHUTU KTK RWANDA YAO (R) UKIZINGATIA MUDA (T) YAANI dR/dT=(TUTSI)t+(HUTU)t]
then,
dR=S(TUTSI)t+(HUTU)t+C
Maana yake ktk lugha ya MAHESABU YA INTEGRAL CALCULUS NI KUWA dR ni Jumla ya kuwaunganisha Watutsi na Wahutu ktk Rwanda yaani S(TUTSI)t+(HUTU)t+C...(S=INTEGRAL SIGN)
Paul Kagame amefanikiwa Kiuchumi lakini Kijamii hasa ktk Mahesabu ya Intergal Calculus hapo juu kuunganisha jamii yake na kuwa kitu kimoja baada ya Kimbari Genocide 1994 amepata ZERO!!!
Duh, hayo mahesabu hapo juu! Ila nimekubali umoja wetu watanzania ni mkuu mno hasa tunapopata "external friction" Rais Kikwete yuko sahihi asilimia 100. Kama wengi walivyosema hapo juu, tatizo la Rwanda ni ardhi na hilo la kukaa mezani kujadili linawatia hofu.
ReplyDelete