Na VOA
Kufuatia wito wa rais Jakaya Kikwete kwa marais wa mataifa ya maziwa Makuu marais Paul Kagame, wa Rwanda, Joseph Kabila wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Yoweri Museveni wa Uganda, kuzungumza na makundi ya waasi yanayopambana na nchi zao, wabunge wa Kongo Kwenye taarifa yao ya pamoja iliyosomwa na mbunge Benjamin Mukulungu , wabunge hao wa Kivu Kusini na Kaskazini wameomba kuwe na mtazamo wa jumla wa viongozi wa kanda ya maziwa makuu na umoja wa mataifa ili kumaliza vita nchini Congo.

Wabunge wa Kivu wamepongeza msimamo wa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wa kutaka kuwe na mazungumzo kati ya serikali za Congo Rwanda na Uganda na makundi ya waasi wanayopingana nayo.

Wabunge wa Kivu wametaka pendekezo la Rais Kikwete ni lazima lipewe kipaumbele na jumuiya ya kimataifa ili kuwe na amani ya kudumu kwenye eneo hilo.

Mbunge wa upinzani Emerio Kunji kutoka jimbo la Kasai amesema amepanga kutoa hoja rasmi bungeni ili kuweko na azimio la bunge kuhusu msimamo ambao serikali ya Congo inatakiwa kuchukua kwa ajili ya kutatua mzozo wa Kivu.

Akisema “Rais wa Tanzania alichukua msimamo wa kijasiri wa kuonyesha kwamba mzozo wa maziwa makuu hauwezi kutambuliwa kwa njia ya kinafiki bali kupitia mtizamo ulio thabiti. Bunge letu ni lazima litoe shinikizo kwa serikali ili kuweko na mtizamo mpya wa ufumbuzi wa mzozo huo”.

Kwa muda wa siku tano sasa pendekeo hilo la rais Kikwete limeendelea kuzusha maoni mengi kwenye vyombo vya habari ngazi ya kisiasa, na kwa watu wa kawaida huko mjini Kinshasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2013

    J.K big up! Umevunja mwiko ambao unalimaliza bara letu la Africa lakuto kuambiana ukweli. Kama kawaida Tz imeendelea kupigania amani ya Africa na uhuru wake. DRC inatakiwa kupata amani ambapo njia pekee ni hayo majambazi kurudi kwao kupitia mazungumzo. Nafurahi kuona Wabunge wa DRC wameliona hilo, this make me happy on the bravity JK has indicated without fear of diplomacy being down graded as reaction from the concerned.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2013

    jembe letu hilo.....

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2013

    huyu mheshimiwa wetu lazima achomoke na tuzo ya Mo Ibrahims akitoka 2015,nani anapinga?King JOJO

    ReplyDelete
  4. Wakati Wakongo wanamsifu JK, Wanyarwanda wana hasira nae sana. Soma hapa http://www.newsofrwanda.com/featured1/18857/understanding-president-kikwetes-sympathy-for-fdlr-rebels/

    ReplyDelete
  5. Wanyarwanada wana hasira sana na JK. Soma hapa http://www.newsofrwanda.com/featured1/18857/understanding-president-kikwetes-sympathy-for-fdlr-rebels/

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 31, 2013

    Big up JK ..umewapa ukweli bana hao wanyarwanda wakitaka wameze au wateme c tunaendelea...JK jembe letu hilo halafu kingine wakileta za kuleta...tutapambana nao pia..kula tano Mh.rais.
    mdau wa London

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 31, 2013

    Mkuu JK ,baba pamba zimekukubali si mchezo ! kweli bongo tambarare kama walivyojiimbia ffu ughaibuni

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2013

    My brother and sister from Tanzania im proud of JK amesema ukweli bunduki haiwezi kuleta amani ya kudumu it is time foor talk my friends mr kagame atake asitake ni lazima akubali ukweli wa wakati umefika ni lazima waongea maneno ya kijinga kutoka kwa huyo waziri wa mambo ya nje akae ajiulize ni miaka mingapi toka waanze kuwafata hawa jamaa mimi ninasema sababu ni veteran nilipiga katika vita ya kuiweka RPF madarakani ila na huyu jamaa kagame alikuwa bosi wangu kule jeshini uganda kabla ajaenda kusoma marekani,baada ya kifo cha fred ndio akarudi ,sasa Jk amesema ukweli wapende wasipende huu ndio ukweli ,wakati umefika kagame na group yake wasifikiri wao ndio wana akili kuliko watu wote kutoka great lake region au wanaona mbali that is the fact mimi ni mtanzania mwenye asili ya kinyarwanda baba mnyarwanda mama muhaya and im proud
    wakati umefika congo lazima ipate amani.
    lubayiza
    Mungu ibariki Tanzania.
    Mungu ibariki Afrika

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 01, 2013

    Ujumbe wameupata kama wana akili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...